Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa shindano la kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanao ‘ Valentine Day’ iliyoandaliwa kwa kushirikiana na Kampuni ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM. Kushoto ni AFISA Masoko na Mauzo wa AMG, Prosper Vedasto
Kampuni ya Push Media Mobile itatoa zawadi ya gari aina ya Vitz lenye thamani ya shs milioni 8 kwa mshindi wa kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanoa “Valentine Day” ikayoa adhimishwa Februari 14.
Hayo yalisemwa na Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo katika uzinduzi wa kampeni hiyi pamoja na Kampuni ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM.
Rugambo alisema kuwa wameamua kutoa zawadi kubwa hiyo ili kuwafanya wapendanao wegi kushiriki na kupata nafasi ya kushinda. Alisema kuwa ili kuingia katika droo ya shindano hilo, unatakiwa kutuma neno “Penzi” kwenda namba 15678 na kujibu maswali mbali mbali yahusiyo masuala ya mapenzi na siku ya Valentine.
“Hii ni promosheni ya kwanza kubwa hapa nchini na mshindi kujishindia gari, lengo kubwa ni kutoa ufahamu kuhusiana na sikukuu ya wapendanao na vile vile kuwazawadia wadau waokwa kushiriki katika shughuli zao za ujenzi wa taifa,” alisema Rugambo.
Alisema kuwa mbali ya zawadi hizo, washiriki wa promosheni hiyo pia watapata nafasi ya kujisha kompyuta (Laptop) aina ya HP yenye thamani ya shs milioni 1.5, simu aina ya Blackberry Curve yenye thamani ya shs 500,000 na Home theatre ya thamani ya shs 400,000 na Ipad.
Kwa mujibu wa Rugambo, lengo lao kubwa ni kuifanya sikukuu ya wapendanao kuwa kubwa kama nyingine kwani mapenzi ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila siku.
Alisema kuwa mipango yao ni kuwekeza katika sikukuu hiyo ambayo jamii imeanza kuitilia mkazo japo si siku ya mapumziko kama sikukuu nyingine. Alisema kuwa kwa mwaka huu, wameweka bajeti ya shs milioni 30 ili kufanikisha zaoezi hilo.
No comments:
Post a Comment