Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ambaye
ndiye Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo tayari ametoa notisi
ya mkutano Mkuu utakaofanyika Februari 23 na 24 mwakani jijini Dar es
Salaam.
Mkutano
huo utafanyika Februari 23 mwakani na kufuatiwa na ajenda ya uchaguzi
siku inayofuata. Ajenda ya uchaguzi iko chini ya Kamati ya Uchaguzi ya
TFF.
Notisi
hiyo imetumwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ambao ni kutoka vyama vya
mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki, klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na
wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.
No comments:
Post a Comment