PAMOJA na
Shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFA) kusema kuwa watafuatilia suala la
wachezaji wao waliogawana pesa za mshindi wa tatu katika mashindano ya chalenji
Uganda, nahodha wa kikosi hicho Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kuwa hatorudisha
pesa hizo kamwe kwani ni haki yake.
Akizungumza jijini leo Cannavaro alisema kuwa pesa hizo zilipatikana kutokana na nguvu
zao katika kufanya vizuri kwenye michuano hiyo na kuweza kuwa washindi wa tatu.
Cannavaro
alisema kuwa kwanza hakutaka kuzigawa pesa hizo kwa wachezaji wenzake, lakini
baadhi yao walikuwa wakimshinikiza kuwapa pesa zao, cha kushangaza wao hao ndio
wamekuwa wa kwanza kuziridisha pesa hizo kwa uongozi wa ZAF.
“Awali mimi
sikuwa na mpango wa kuzigawa pesa hizo, lakini kutokana na wao wenyewe kutaka
pesa zao, nililazimika kuwagawia lakini leo wao ndio wa kwanza kuogopa na
kuzirudisha pesa hizo kwa ZFA,” alisema Cannavaro.
Alisema kuwa
kwa maana hiyo anaweza kuwaita wasaliti kutokana na kitendo walichikifanya
kwani yeye hataogopa kitu chochote na hawezi kuzirejesha pesa hizo ZAF.
Aliongeza
kuwa hata kama uongozi wa ZFA wakipeleka taarifa hizo TFF, wao hawahusiki na
chochote kwani suala hilo limefanyika Ugana na linahusina na wachezaji wa
Zanzibar na sio Tanzania Bara.
“Hata kama
wakileta mashitaka hayo TFF haitasaidia kitu kwani suala hili linahusisha
wachezaji wa Zanzibar na halijatokea huku Bara,” alisema Cannvaro.
No comments:
Post a Comment