Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, November 4, 2012

YANGA YAISHUSHA SIMBA KILELENI BAADA YA ICE CREAM ZA AZAM KUYEYUKA JANGWANI NA SIMBA KUKUBALI KUBEBA MAGUNIA MAWILI YA SUKARI YA MTIBWA MOROGORO










TIMU ya Yanga leo imeipiku Simba  kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuifunga Azam FC mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Ushindi huu, unaifanya Yanga iongoze Ligi kwa kufikisha pointi 26, ikiwa imebakiza mechi moja kumaliza mzunguko wa ambao itacheza na Coastal Union ya jijini Tanga.

Simba yenye pointi 23,leo imefungwa 2-0 na Mtibwa Sugar mjini Morogoro. 
Hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbangu aliyeunganisha krosi ya Simon Msuva kutoka wingi ya kulia dakika ya tisa.

Mabeki wa Yanga walicheza vema na kuweza kumdhibiti mshambuliaji hatari wa Azam mwenye uchu wa mabao, John Bocco ‘Adebayor’
Hamisi Kiiza aliifungia Yanga bao la pili dakika ya 68, akiunganisha krosi ya Athumani Iddi ‘Chuji’ kutoka wingi ya kulia.
Baada ya kufunga bao hilo, Kiiza alivua jezi yake na kubaki na fulana ya njano yenye maandishi; Rest In Peace Mafisango, I miss you So much my brother, akimaanisha kumwenzi aliyekuwa kiungo wa Simba, Patrick Mutesa ambaye alifariki dunia kwa ajali ya gari Mei mwaka huu.


Kikosi cha Yanga; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo, Simon Msuva, Hamisi Kiiza, Haruna Niyonzima na Didier Kavumbangu.

Azam FC; Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Ibrahim Shikanda, Aggrey Morris na Said Mourad, Jabir Aziz, Kipre Balou, Khamis Mcha, Salum Abubakar, John Bocco na Kipre Tcheche.

No comments:

Post a Comment