Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 9, 2012

TIMU ZA POLISI ZASHINDWA KUONESHA MAKUCHA LIGI DARAJA LA KWANZA

TIMU ya Kanembwa ya Kigoma juzi iliifunga Polisi Tabora mabao 4-1 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora

Kanembwa ambayo mpaka sasa ndio inaongoza kundi C ilijipatia mabao yake kupitia kwa Ali Bilal aliyefunga hat-trick dakika za 46, 60 na 89 na Baruani Akilimalui dakika ya 49.

Polisi Tabora ambayo inaonekana kuchechemea ilijipatia bao hilo la kufuta machozi kupitia kwa Ibrahimu Musa dakika ya 86.

Kwenye uwanja wa CCM Kirumba timu ya Pamba waliweza kuutumia vema uwanja wa nyumbani kwa kuifunga Moran ya Kiteto 3-0.

Uwanja wa Jamhuri Polisi Dodoma na Polisi Mara walitoka suluhu ya bila kufungana.

Ligi iliendelea kwa kundi A kuchezwa michezo miwili, kwenye uwanja wa Majimaji wenyeji Mlale waliweza kuondoka na pointi tatu kwa kuifunga Polisi Iringa bao 1-0.

Huko Mbeya uwanja wa Sokoine  wenyeji Mbeya City waliifunga Kurugenzi mabao 3-0.

Mabao ya Mbeya City yalifungwa na Alex Seth dakika ya 34, Patrick Mangunguru dakika ya 80 na Haruni Mohamedi dakika za nyongeza (dakika 92)

No comments:

Post a Comment