TIMU ya Small Kids ya Rukwa inayoshiriki daraja la kwanza imekuwa timu ya kwanza kushuka daraja baada ya kushindwa kufika kwenye viwanja kwa michezo miwili.
Small kids ambayo ilikuwa kama msindikizaji kutokana na kufungwa michezo yote ni sawa na imejishusha kwani haikufika kwenye mchezo mjini Mafinga dhidi ya Kurugenzi na juzi nyumbani kwao Rukwa dhidi ya Polisi Iringa.
Kulingana na kanuni za ligi ya Tanzania, timu isipofika uwanjani itakuwa imejishusha daraja yenyewe ikifuatiwa na kupigwa faini na kufutwa kwa pointi zote za michezo ambayo ilikuwa imecheza.
Wachezaji wa Small Kids ambao ni wenyeji wa Dar es Salaam walirejea jijini baada ya mchezo wao na Burkina Faso uliochezwa mjini Morogoro kwenye uwanja wa Jamhuri ambapo pia walifungwa bao 2-0.
Wenyeji wa Rukwa wamesikitishwa na kitendo cha mmiliki wa Small kids kushindwa kusimamia timu na kusambaratika kabla ya ligi hata kuamaliza mzunguko wa kwanza.
No comments:
Post a Comment