Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, November 5, 2012

SERENGETI BOYS KUCHEZA NA BOTSWANA MECHI YA KIRAFIKI




TIMU ya Vijana waliochini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti boys wanatarajia kuondoka nchini Novemba 11 mwaka huu kwenda nchini Botswana kucheza michezo ya kirafiki ya kimataifa.

Akizungumza  jijini leo kocha Msaidizi wa timu hiyo Jamhuri Kiwelu "Julio" alisema wakiwa nchini Botswana watacheza michezo miwiliya kirafiki.

Mchezo wa kwanza wanatarajiwa kucheza na Botswana Novemba 12 au 13 na mchezo mwingine watacheza na Angola Novemba 13 au 14.

"Tutasafiri kwenye Botswana kucheza michezo ya miwili ya kirafiki nchini Botswana ambapo tutacheza na wenyeji Botswana na utakaofuata tutacheza na Angola hapohapo Botswana", alisema Julio

Pia alisema kama muda utaruhusu inawezekana wakacheza mchezo mwingine na Afrika ya Kusini.

Timu hii ambayo inakabiliwa na mchezo wa kutafuta kufuzu fainali za vijana dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo utakaochezwa nyumbani kati ya Novemba 17 na 18 mwaka huu.

Kikosi cha wachezaji wa timu hii kinaonekana kuwa na morali sana ya ushindi na wanasema watahakikisha wamefuzu kuiwakilisha Tanzania kwenye fainali zitakazofanyika nchini Morroco, Machi mwakani.

No comments:

Post a Comment