Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, November 10, 2012

MORO UNITED NA GREEN WORRIORS ZATOKA SARE


Mshambuliaji Joseph Mhagama wa Green Worriors akiwa amekabwa na beki Awadh Mohamed wa Moro United kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Karume

Beki Ramadhan Musa wa Moro United akimtoka mshambuliaji wa Green Worriors Joseph Mhagama kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Karume jana na timu zote zilitoka sare ya 1-1.

TIMU za Moro United na Green Worriors za Dar es salaam jana zilishindwa kuonyeshana ubabe baada ya kutoka suluhu kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Karume.

Mchezo huu ulikuwa wa ushindani sana lakini iliichukua dakika 15 tu Green Warriors kujipatia bao kupitia kwa Adamu Seif Said kwa shuti la mbali.

Moro United nao dakika ya 25 walisawazisha bao kwa njia ya penalti lililofungwa na nahodha wao Oraph Mwamlima.

Kwa mchezo huu ni kama Moro United wamezinduka maana ina pointi moja baada ya kufungwa michezo minne iliyopita.

Uwanja wa Mabatini Villa Squad walipokea kichapo cha 2-0 kutoka kwa wanajeshi wa Transit Camp.

Transit Camp walitawala sana mchezo huo na kuwafanya vijana wa Magomeni (Villa) kutafutana uwanjani.

Kundi A ulichezwa mchezo mmoja kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, kati ya Burkina Faso na Small Kids.

Burkina Faso waliifunga Small Kids mabao 2-0, mabao ambayo yalipatika kipindi cha pili.

No comments:

Post a Comment