Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, November 15, 2012

DSTV YATOA PUNGUZO ASILIMIA 10 KUANZIA LEO

Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania, Peter Fauel akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Holiday Inn, jijini Dar es Salaam, kuhusu punguzo la asilimia 10 ya malipo ya mwezi kwa wateja wa televisheni kwa vipindi vya DStv litakaloanza leo, kulia ni afisa uhusiano wa DStv Barbara Kamboji.







KAMPUNI ya Multichoice imetoa punguzo la asilimia 10 ya malipo ya mwezi kwa wateja wa televisheni kwa vipindi vya DStv linaloanza leo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania, Peter Fauel alisema punguzo hilo litawezesha wateja wao kulipia huduma za matangazo ya televisheni ya kituo hicho kwa gharama nafuu.

Fauel alisema wateja watakaokuwa wamelipia huduma hiyo ndani ya mwezi huu, wataendelea kutumia hadi pale mwezi utakapokuwa umeisha, kisha wataanza na bei mpya ya punguzo kuanzia mwezi unaofuata ila wahakikishe huduma yao kutokatika.

"Tumedhamiria kuwapunguzia wateja wetu gharama kubwa kulingana na hali halisi ya maisha ya mwananchi wa kawaida", alisema Fauel.

Pia alisema ni kawaida yao kuwapa wateja wao unafuu wa bei kulingana na kipato chao, hivyo punguzo hili litawanufaisha kwa kiwango kikubwa kila mmoja ili afaidi vipindi vyenye ubora kwa vile wamewekeza kwenye vipindi vipya.

Wateja watakaonufaika na ofa hii wataweza kupunguza gharama za kulipia huduma yao ya DStv kwa mwaka.

Fauel aliongeza kuwa mtandao wao wa usambazaji unazidi kupanuka na sasa wapo kila mkoa nchini ili kuwarahisishia wateja kupata huduma na bidhaa zao kwa haraka zaidi.

No comments:

Post a Comment