MSHAMBULIAJI wa zamani
wa Chelsea, Didier Drogba amekiri kwamba amekuwa akitumia meseji usiku wa
manane kutoka kwa kocha wake wa zamani Jose Mourinho.
Drogba, ambaye kwa sasa anacheza soka nchini
China, kwenye klabu ya Shanghai Shenua, alisema kwamba ataendelea kuwa karibu
na Mourinho na Roman Abramovich, milele na ndio maana wameendela kuwasiliana.
“Lakini tatizo la Jose
(Mourinho), bado hajajua kama kuna tofauti ya muda kati ya China na Hispania na
amekuwa akinitumia meseji usiku wa manane nikiwa nimelala.” Alisema Drogba.
No comments:
Post a Comment