BONDIA Floyd Mayweather ameendelea kuweka rekodi ya kucheza mapambano 50 bila kupoteza baada ya kumpiga Conor McGregor katika pambano la ubingwa wa dunia kwa Knockout ‘KO’ raundi ya 10 jijini Las Vegas.
Katika mapambano hayo 50, Mayweather alishinda 27 kwa knockout huku 23 akifanikiwa kuibuka mshindi kwa idadi ya pointi.
McGregor alianza pambano hilo kwa kasi ambapo katika raundi mbili za mwanzo alirusha ngumi ambazo huku Mayweather akionekana kutojibu mashambulizi lakini kuanzia raundi ya saba mambo yalibadilika kwa raia huyo wa Ireland kwa kupokea makonde mazito.
“Nilitaka mwamuzi aniache niendelee kumshushia makonde. Nilikuwa na uchovu kidogo mwanzoni hilo nalo lilimsaidia,” alisema McGregor.
Pambano hilo lilihudhuriwa na mamia ya mashabiki nchini Marekani huku likitazamwa pia kutoka sehemu mbalimbali za dunia kupitia runinga pamoja na mitandao ya kijamii.
Myweather amepata kitita cha dola 300 milioni ambazo ni karibia sh 700 bilioni za kitanzania huku akistaafu masumbwi baada ya kumalizika kwa pambano hilo.
No comments:
Post a Comment