WANARIADHA WA MADOLA KURUDI KESHO

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Tanzania
iliyoshiriki Michezo ya sita ya Jumuiya ya Madola kwa vijana na kutwaa medali
ya shaba inatarajia kutua nchini keshokutwa Alhamisi kutoka Nassau, Bahamas.
Mwanariadha Francis
Damas alitwaa medali hiyo baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu katika mchezo
wa mbio za meta 3,000 kwa kutumia dakika 8.37.51 nyuma ya Mkenya na Mcanada
walimaliza katika nafasi ya kwanza na pili.
Katibu Mkuu wa
Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi alisema jana kuwa, timu hiyo
yenye wanariadha wawili na waogeleaji wawili, itatua nchini majira ya mchana
kwa ndege ya Emerates.
Kwa medali hiyo,
Damas anakuwa Mtanzania wa pili kutwaa medali kutoka katika michezo hiyo baada
ya Mary Naali aliyetwaa medali kama hiyo katika michezo ya mwaka 2008
iliyofanyika Pune, India kwa upande wa wanawake.
Tangu wakati huo
Tanzania haijawahi kutwaa medali kutoka katika michezo iliyofuata ya mwaka 2011
huko Iron Man, Marekani, ambako hatukushiriki na ile ya Samoa (2015), tulitoka
mikono mitupu.
Mbali na kutwaa
medali, mwanariadha mwingine wa Tanzania Reginal Mpigachai ambaye alitinga
fainali ya mbio za meta 800 licha ya kumaliza katika nafasi ya nane, aliboresha
tena muda wake binafsi.

Mpigachai awali
katika hatua ya nusu fainali alimaliza watano kwa kutumia dakika 2.11.65 na
kuboresha muda waka bora wa awali wa dakika 2.13.51 aliouweka katika mashindano
ya Kanda ya Tano ya Afrika yaliyofanyika jijini Dar es Salam.
Katika fainali za
meta 800, Mpigachai alimaliza katika nafasi ya nane, huku akitumia dakika
2.10.57 na kuboresha zaidi muda wake bora.

Post a Comment