Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, June 1, 2017

WENGER NDIYE ‘STERLING’ EMIRATES TU, AONDOKE VIPI



 Image result for WENGER
JUMANNE jioni watu walikuwa wamejikusanya katika makundi madogo na wengine makubwa hapa Kaskazini mwa London, wakijadili uamuzi wa Arsene Wenger kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kubaki klabuni hapa.
Amechukua uamuzi huo, ikiwa ni kipindi kifupi kabisa tangu kuwatandika Chelsea 2-1 na kutwaa Kombe la FA, lakini ikiwa pia si muda mwingi tangu kwa mara ya kwanza katika miongo miwili wamalize Ligi kuu ya England (EPL) nje ya nne bora za juu.
Hii inamaanisha nini? Kwa mara ya kwanza Arsenal hawashiriki msimu ujao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL), kwa mara ya kwanza wamemaliza kwenye nafasi ya tano, kwa mara ya kwanza shinikizo kubwa limekuwa kwa Mfaransa huyo kuondoka.
Lakini kwa mara nyingine tena ameonesha yeye ndiye ndiye ‘sterling’ hapo Emirates na atakwenda kwa zaidi ya miaka 22 mfululizo, akiwa pia mtoa uamuzi wa kipi kifanyike.
 Alikutana na mmiliki wa Arsenal, Mmarekani Stan Kroenke Jumatatu, akakubali ofa aliyokuwa amewekewa mezani kitambo sasa.
Baada ya kumalizana wawili hao, kilichofuata ni kupeleka tu uamuzi huo kwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Arsenal waliokuwa wakikutana juzi Jumanne kwa kikao cha kawaida cha mwaka, ikiwa pamoja na mambo mengine ilikuwa kuona mwelekeo wa klabu hiyo.
Baada ya kumaliza Ligi Kuu wakiwa pointi 18 nyuma ya mabingwa wapya Chelsea, huku vijana wa Stamford Bridge wanaofundishwa na Antonio Conte wakiwa kwenye kiwango cha juu, walitabiriwa kuchukua pia Kombe la FA, lakini kama walivyofanya kwa Manchester United kwenye mechi ya EPL, Arsenal waliwanyamazisha Chelsea kwa mabao mawili tena.
Wenger ameweka historia ya kuwa kocha mwenye mafanikio zaidi katika rekodi za Kombe la FA, kwani amelitwaa mara nne kati ya saba ambazo Arsenal wamelichukua, lakini pia amewapa ubingwa wa England mara tatu.
Ni wazi anaamini kwamba alitakiwa aheshimiwe zaidi na washabiki, lakini pia wamiliki na viongozi kuweka zaidi imani kwake.
Iwapo Arsenal wangefungwa na Chelsea, tena wakafungwa kwa idadi kubwa kabisa ya mabao kama wengi walivyotarajia, basi kungekuwa na giza kubwa klabuni, giza ambalo huenda ingekuwa vigumu hata kwa washabiki wanaomuunga mkono kuendelea kusimama naye.
Badala yake, tafsiri inayokuja kwa ushindi wa Arsenal dhidi ya Chelsea ni kwamba bado Wenger ana uwezo wa kushinda mechi kubwa – gemu ngumu na anaweza kutoa majibu kwa maswali magumu.
Moja ya mbinu mpya alizokuja nazo kwenye mechi za mwisho, ni zile alizoziua alipoingia Arsenal 1996 – matumizi ya beki tatu. Amerejea kule na kusema kwamba hata katika umri wake mkubwa, bado anaweza kukumbatia mageuzi.
Bila shaka kwenye kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa Arsenal, ingetokea ubishani basi angewaonesha Kombe la FA na kuwaeleza kwamba ndio ushahidi wa wazi kwamba bado ana uwezo wa kufanya mambo Emirates dhidi ya klabu kubwa.
Sasa kama Wenger ameshaamua kubaki, anatakiwa kuharakisha masuala ya wachezaji wake nyota, Alexis Sanchez na Mesut Ozil yanamalizwa kwa njia chanya kwa klabu. Tunasikia jinsi Manchester City na Bayern Munich wanavyomuwania Sanchez huku Ozil akidaiwa kupigwa jicho na Besiktas wa Uturuki.
Pale Wembley dhidi ya cheslea, wawili hao walicheza vyema, wakawa kwenye viwango vizuri na kuonesha uzalendo mkubwa kwa klabu, hivyo ni juu ya Arsenal sasa kuonesha nguvu na kuamua kuwabakisha Emirates.
Wenger akishawatuliza hao, inabidi awageukie Waingereza Alex Oxlade-Chamberlain na Theo Walcott, ambao hapana ubishi kwamba wana vipaji sana, lakini hawajaonesha kazi ya ufanisi kwa uendelevu sana.
Kabla ya kuukubali mkataba mpya, Wenger alisikika akisema kwamba Washika Bunduki wa London wanahitaji mchezaji mmoja au wawili tu wapya wenye kiwango cha juu kabisa, lakini lazima wawe timamu kiakili na kimwili, ili kuepuka kuanguka anguko kubwa kama lile lililoanza Machi mwaka huu na kuwagharimu nafasi ‘yao’ UCL.

No comments:

Post a Comment