Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF ) Bw.
Jumanne Mbepo, ambao ndo wadhamini wakuu wa mbio za Rock City Marathon
2014, akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika
Jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika
uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Bw. Dioniz Malinzi, amezindua
rasmi mbio za Rock City Marathon, zitakazofanyika Oktoba 26 mwaka huu
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Akizungumza
katika uzinduzi huo jana jijini Dar es Salaam, Malinzi alisema mbio
hizo zimeweza kuwa ni moja ya mbio zinazoheshimika nchini Tanzania na
kuiweka kanda ya ziwa katika kalenda ya michezo kila mwaka.
Malinzi
aliipongeza kampuni ya Capital Plus International (CPI) kwa kuendelea
kujidhatiti katika maandalizi ya mbio hizo na kuziboresha kila mwaka
licha ya changamoto nyingi zinazoukabili mchezo huo wa riadha nchini.
“Ni
kweli kwamba makampuni na hata watu binafsi wamekuwa wakisaidia kukuza
mchezo wa riadha hapa nchini, lakini bado mchezo huu unachangamoto
nyingi.
“Jitihada
za pamoja zinahitajika baina ya serikali kupitia Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, sisi Baraza la Michezo la Taifa (BMT),
vyama vya michezo, mashirika na wadau wengine, ili kurejesha heshima
iliyopotea miongoni mwa michezo na wanamichezo wa Tanzania, hususani
riadha,” alisema Bw. Malinzi.
Bw.
Malinzi alibainisha kuwa na kuwepo kwa changamoto mbali mbali CPI
imekuwa ikijitahidi kuboresha mbio hizo zifanyikazo kila mwaka.
“Tumeshuhudia
viwango vya mbio hizi vikipanda kila mwaka, ambapo ni kielelezo cha
maandalizi mazuri yanayofanywa kwa kuzingatia viwango na sheria zilizo
wekwa,” aliongeza Bw. Malinzi.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui
akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika Jijini
Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika
uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Hata
hivyo, Mwenyekiti huyo wa BMT alisisitiza kuwa vyama vya michezo pia
vinapaswa kujiimarisha katika kuwaandaa wachezaji kabla ya kuwapeleka
kushiriki katika mashindano ya kimataifa ambapo wachezaji hao wanabeba
jina la nchi ya Tanzania.
“Hatunabudi
kuimarisha msingi wetu katika kila aina ya michezo hapa nchini, kama
bado tunayo ndoto ya kuirudisha ramani ya Tanzania katika ulimwengu wa
michezo kama ilivyokuwa zamani,” alisisitiza.
Tukio
hilo limewavutia wadau wengi wa michezo nchini, ikiwa ni pamoja na
makampuni makubwa kama Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Kampuni ya TSN Group Ltd, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), African Barrick
Gold, Nyanza Bottlers, Mfuko wa Pensions (PPF), Sahara Communication,
ATCL, New Mwanza Hotel, na New Africa Hotel ambao wamejitokeza kudhamini
mbio hizo.
Afisa
Uhusiano na mawasiliano wa TSN Group Koiya Kibanga, ambao ni moja
wa wadhamini wakuu wa mbio za Rock City Marathon 2014, akizungumza
machache wakati wa uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika Jijini Dar es
Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba. katika uwanja wa
CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa kampuni ya Capital Plus International, Bw.
Mathew Kasonta, alisema mbio za mwaka huu zitahusisha mbio za nusu
Marathon za kilomita 21, mbio za kujifurahisha maarufu kama Corporate
Race za kilomita 5, mbio za watu wenye ulemavu wa ngozi za kilomita 3,
mbio za watu wazima za kilomita 3 na mbio za watoto kuanzia miaka saba
hadi 10 ambazo ni za kilomita 2.
Bw.
Kasonta alisema kuwa mbio hizo zinaenda sambamba na kuhamasisha Utalii
wa ndani kupitia sekta ya michezo, ambapo washiriki watakua ni kutoka
kanda ya ziwa Victoria na nchi jirani kama Kenya, Uganda, Afrika Kusini
na baadhi yao wakiwa na uzoefu wa kucheza mashindano ya kimataifa ili
kutoa ushindani zaidi.
“Ningependa
kutoa shukrani zangu za dhati kwa wafadhili mbalimbali wanaoshirikiana
nasi ili kuyafanikisha mashindano haya, kwa niaba ya Capital Plus
International, ningependa kuwahakikishia kuwa mashindano ya mwaka huu
yataboreshwa zaidi na hivyo yataweza kutupatia wanariadha bora
watakaoiwakilisha nchi yetu kikamirifu katika mashindano ya kimataifa,”
alisema Bw. Kasonta.
Msemaji
wa Kampuni ya Capital Plus International, ambao ni waandaaji wa mbio za
Rock City Marathon, Bw. Mathew Kasonta, akizungumuza na wageni waalikwa
katika uzinduzi wa mbio hizo jana iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza.
Baadhi
ya wawakilishi wa wadhamini wa mbio za Rock City Marathon 2014 pamoja
na viongozi wa chama cha mchezo wa riadha Tanzania, wakifuatilia
yanayojiri wakati wa uzinduzi wa mbio hizo jana iliyofanyika Jijini Dar
es Salaam. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza.
Mratibu
wa Rock City Marathon kutoka kampuni ya Capital Plus International
Ltd, Bi Grace Sanga (wa kwanza kulia) akipongezwa na Mwenyekiti wa
Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Bw. Dioniz Malinzi (Wa nne kulia)
ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Rock City Marathon 2014,
jana jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba
katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.( Picha na mpiga picha
wetu).
No comments:
Post a Comment