
Man United wako Nafasi ya 6, Pointi sawa na Tottenham, wote wakiwa na Pointi 34 ikiwa ni Pointi 8 nyuma ya Vinara Arsenal lakini ni Pointi 2 tu nyuma ya Timu ya 5 Liverpool ambao nao wako Pointi 1 nyuma ya Everton walio Nafasi ya 4.

Wakati Timu zote, Man United na Spurs, zikiwa zimeanza Msimu vibaya kwa Man United kufungwa Mechi 5 kati ya 15 za kwanza za Ligi na Tottenham kumtimua Meneja wao Andre Villas-Boas, hivi karibuni Timu hizo zimeanza kufanya vizuri.

Man United wameshinda Mechi zao 6 zilizopita katika Mashindano yote wakati Tottenham, chini ya Meneja mpya Tim Sherwood, ambae hutumia Mfumo wa 4-4-2, hawajafungwa Mechi ya Ligi tangu atwae himaya Wiki mbili zilizopita.

Kwenye Mechi hii, Man United wanatarajiwa kuwa nae Wayne Rooney ambae aliikosa Mechi Jumamosi waliyowafunga Norwich City Bao 1-0 baada kupona maumivu ya Nyonga lakini huenda wakamkosa Robin van Persie, ambae, licha ya kupona majeruhi yake na kuanza Mazoezi, huenda akawa si fiti kwa Mechi baada kuwa nje Mwezi mzima.




Santi Cazorla yupo pamoja na kupata maneno maneno kutoka kwa Per Mertesacker

Podolskinae yupo

RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumatano Januari 1
15:45 Swansea vs Man City
18:00 Arsenal vs Cardiff
18:00 Crystal Palace vs Norwich
18:00 Fulham vs West Ham
18:00 Liverpool vs Hull
18:00 Southampton vs Chelsea
18:00 Stoke vs Everton
18:00 Sunderland vs Aston Villa
18:00 West Brom vs Newcastle
20:30 Man United vs Tottenham
No comments:
Post a Comment