Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, April 3, 2013

PAOLO DI CANIO AGOMA KUJIBU MASWALI YA KIZUSHI YA WAANDISHI WA HABARI JUU YA SIASA ZAKE ZA UFASHISTI




Meneja mpya wa Sunderland Paolo Di Canio amekataa kujibu swali aliloulizwa kuhusiana na kama anaikumbatia imani yake ya kifashisti katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari akiwa bosi mpya wa Sunderland.

Bosi huyo mtaliano ameelezea juu ya gumzo kubwa lililoibuka juu ya kuteuliwa kwake kuwa meneja wa Sunderland akichukua nafasi ya Martin O’ Neil kuwa ni jambo la kuchekesha na pia la kusikitisha.

Kuhusina na kujiuzulu kwa katibu wa zamani na makamu wa mwenyekiti David Miliband amesema hili ni jambo la kisiasa na kwamba hakuwa na majibu juu ya swali hilo.

Di Canio alikataa kuzungumzia juu ya siasa huku akisema kuwa yeye si mwanasiasa na hayuko bungeni kujibu mambo hayo na kwamba angeweza kujibu maswali yanayo husu soka.

Di Canio aliripotiwa katika mahojiano na shirika la habari la Ansa mwaka 2005 kuwa saluti aliyopiga wakati huo akichezea Lazio ilikuwa ni maalum kwa watu wake ambao walikuwa wakimfuata Benito Mussolini ambaye alikuwa akiongoza harakati za mafashisti  na kwamba halikuwa kwa lengo la ubaguzi.

No comments:

Post a Comment