Meneja Mkuu wa kampuni ya JP Decaux Ltd, Bwana Shaban Makugaya (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu tamasha la bodabodaDar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa JP Decaux Ltd, Bwana Elias Richard. |
KATIKA
kukabiliana na ajali za pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam, Kampuni ya JP Decaux
Tanzania wakishirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la International
Republican Institute (IRI) wameandaa tamasha kwa ajili ya kutoa elimu kwa
waendesha pikipiki.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini hapa,
Mkurugenzi Mtendaji wa JP Decaux, Shabani Makunganya alisema tamasha hilo
maalumu kwa wadau wa pikipiki litakaloitwa ‘Dar Bodaboda Superstar’ litafanyika
Mei 17 mwaka huu, Dar es Salaam.
Alisema
lengo la tamasha hilo ni kuweka msisitizo na kuendelea kutoa elimu ya usalama
barabarani kwa madereva wa pikipiki na abiria kwa dhumuni la kuzingatia sheria
za usalama na matumizi ya barabara kwa ujumla sambamba na msisitizo wa kuwa na
nidhamu ya kazi na juhudi ili kupata maendeleo.
“Tumeona
kuna umuhimu wa waendesha pikipiki kupatiwa elimu juu ya usalama wao tayari
tumeshatoa taarifa kwa jeshi la polisi usalama barabarani kwa ajili ya
kushirikiana nao,”alisema Makunganya.
Alisema
tamasha hili linatarajia kushirikisha waendesha pikipiki 5,000 kwa mkoa wa Dar
es Salaam na baadaye watakwenda katika mikoa mingine, lengo ni elimu hiyo
kufika kwa waendesha pikipiki wengi zaidi.
Aidha
alisema wameamua kutoa elimu hiyo kwa waendesha pikipiki kwa kuwa usafiri huo
umekuwa ni kati ya njia rahisi ya kumuwezesha msafiri kufika haraka hata pale
inapotokea dharura.
“Licha ya
manufaa ya usafiri huo ila ni wazi kuwa usafiri huo umekuwa unaongoza kwa
kupata ajali zinazopelekea kupoteza maisha ya watu wengi sambamba na kuhusishwa
na matukio ya uhalifu nchini, hivyo ni muhimu elimu hii kutolewa,”aliongeza.
No comments:
Post a Comment