Kikosi cha
wachezaji 22 cha Yanga kimeondoka kwenda Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Kombe la
Shirikisho (FA) nusu fainali dhidi ya Mbao FC utakaochezwa Jumapili ya wiki hii
Katibu Mkuu
wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amewataja wachezaji wanaotarajiwa kuondoka ni
makipa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Benno Kakolanya na Ally Mustafa ‘Barthez’,
mabeki Oscar Joshua, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Hassan Kessy, Kevin Yondan,
Andrew Vincent na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Viungo ni
Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Said Juma ‘Makapu’, Juma
Mahadhi, Simon Msuva, Geoffrey Mwashiuya, Obrey Chirwa na Emmanuel Martin
wakati washambuliaji ni Amissi Tambwe na Matheo Antony.
Wachezaji wanne watakosekana beki Vincent Bossou, kiungo Yussuf Mhilu na washambuliaji Malimi Busungu na Donald Ngoma.
Bossou, Ngoma na Busungu ni majeruhi, wakati Mhilu yupo na kikosi cha timu ya vijana cha timu hiyo, ambacho jana kilitoa sare ya 1-1 na Kombaini ya timu ya Majeshi mjini Dodoma.
Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la ASFC inatarajiwa kuchezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Azam FC na Simba SC.
Ikumbukwe Yanga SC ndiyo mabingwa watetezi wa Kombe la TFF baada ya kuifunga Azam 3-0 katika fainali mwaka jana.
Mara tu baada ya mchezo huo, Yanga inatarajiwa kurejea Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Prisons ya Mbeya.

Kocha
Msaidizi Juma Mwambusi amesema kikosi chake kiko vizuri na tayari kwa mchezo
huo wa Jumapili.
Alisema
wanauchukulia kama fainali wakiamini ushindi utawawezesha kusonga mbele na
kucheza fainali kwa mara ya pili baada ya kuchukuwa ubingwa msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment