TIMU ya wavu ya Jeshi Stars imefanikiwa kutetea kombe
la mashindano ya Muungano baada ya kuifunga Tanzania Prisons kwa seti 3-1 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye
Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.
Jeshi Stars
ambayo msimu uliopita ilicheza fainali na Mafunzo, nyota yake ilionekana
kung’aa mapema kwani seti ya kwanza walimaliza kwa 25-13, seti ya pili 25-18,
seti ya pili 22-25 na seti ya nne 25-15.
Jeshi Stars
ilifuzu fainali baada ya kuifunga Chui kwa seti 3-1 katika mchezo wa nusu
fainali ya kwanza ambapo seti ya kwanza ilishinda kwa 25-21, 23-25, 25-22 na
25-18
Tanzania
Prisons iliifunga Mafunzo kwa seti 3-0 ambapo seti ya kwanza ilishinda 25-21,
seti ya pili 25-23 na seti ya tatu 25 -20.
Kwa upande
wa wanawake Tanzania Prisons imeibuka bingwa baada ya kuizidi Jeshi Stars kwa kushinda
seti nyingi kuliko Jeshi Stars lakini kila moja ikiwa na pointi tisa kwa sababu
walicheza kwa mfumo wa ligi
Akizungumza
na gazeti hili, Katibu Msaidizi wa TAVA, Alfred Selengia alisema mashindano yalikuwa
na ushindani na idadi ya timu zimeongezeka tofauti na miaka ya nyuma na
kufanikiwa kuchangua timu ya taifa ya wanawake na wanaume pia ya U-20.
“Mashindano
yalikuwa na ushindani na wachezaji walionesha uwezo mkubwa na kupitia mashindano
haya tumepata wachezaji 36 wa timu za Taifa za wanawake, wanaume nay a vijana
ya U-20,” alisema Selengia
Pia Selengia
alisema bingwa ndie atawakilisha nchi kwenye mashindano ya Afrika ambayo
yatafanyika mwakani kwa timu za wanawake na wanaume
Timu zinazoshiriki
ni bingwa mtetezi Jeshi Stars, Chui, Polisi Zanzibar, Moro Stars, Makongo
sekondari, Tanzania Prisons, Saut Mwanza, Mafunzo ya Zanzibar, Dodoma,
Mjimwema, Victory Sports na Kinyerezi.
Timu za
wanawake ni Tanzania Prisons, Jeshi Stars, Shule ya Sekondari ya Makongo, Saut
ya Mwanza, Mjimwema na Dodoma.
No comments:
Post a Comment