Thursday, April 27, 2017
DK TULIA KUFUNGUA MAFUNZO TaSUBa JUMAMOSI
TAASISI ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa kushirikiana na Tulia Trust kesho wanatarajia kuzindua mafunzo maalumu ya Sanaa kwa vijana 27 kutoka Mkoani Mbeya, katika ukumbi wa maonyesho wa TaSUBa, wilayani Bagamoyo, Pwani.
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk.Tulia Ackson Mwansasu (Mb).
Akizungumza na gazeti hili, Mtendaji Mkuu wa TaSUBa, Dk. Herbert Makoye alisema vijana hao 27wanatoka wilaya za Rungwe, Busokelo na Kyela, Mkoa wa Mbeya na wamefadhiliwa na Dk. Tulia ambaye ni mwanzilishi wa Tulia Trust.
“Vijana hao wamefadhiliwa gharama za mafunzo ambazo ni ada, malazi, chakula na usafiri ili kupata elimu maalum ya Sanaa na Utamaduni na tayari wapo Bagamoyo,” alisema Dk. Makoye.
Mafunzo hayo yamegawajika katika awamu mbili; awamu ya kwanza ina vijana 20 ambao tayari wameishaanza mafunzo maalumu kwa muda wa miezi miwili ambayo yatahusisha kujifunza uchezaji ngoma za asili ya Tanzania, ngoma za ubunifu, muziki wa asili ya Tanzania, uigizaji, matumizi ya jukwaa na maleba.
Awamu ya pili itahusisha vijana saba ambao watapata mafunzo katika ngazi ya stashahada na Astashahada katika fani za sanaa za maonyesho na ufundi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment