Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, October 6, 2019

TANZANIA BARA BINGWA WA KWANZA WA MASHINDANO YA CHALENJI YA U20


Image
Image ya Taifa ya Tanzania Bara U20 imeibuka bingwa wa mashindano ya CECAFA baada ya kuifunga timu ya Kenya kwa bao 1-0 katika mchezo uliochwezwa kwenye Uwanja wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA Technical Centre) uliopo Njeru, Jinga na Eritrea ikishika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Sudan 1-0
Katika mchezo huo ambao ulijaa ufundi Tanzania Bara ilipata bao katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza baada ya mchezaji wa Kenya John Ochieng kujifunga na kuifanya kwenda mapumziko ikiwa mbele.
Baada ya kutoka mapumziko Kenya walifanya mabadiliko ya kumtoa Ronald Sichenje na kuingia  Benson  Ochieng  dakika ya 50 na dakika ya 65 Tanzania Bara ilimtoa  mshambuliaji Luyaya Said  na kuingia Andrew Albart na kufanya kila timu kuongeza mashambulizi.
Akizungumza baada ya mchezo Kocha Zuberi Katwila alisema waliingia kwenye mchezo wakijua wanakwenda kushinda kwa sababu walishawasoma Kenya wanavyocheza.
“Namshukuru Mungu kwa sisi kuwa mabingwa lakini tuliingia kwenye mchezo tukijua tunakwenda kushinda kwa sababu tulishaisoma Kenya jinsi wanavyocheza kwani hata hatua ya makundi tulitoka nao sare ya mabao 2-2,” alisema Katwila
Katika mashindano hayo Kelvin John wa Tanzania Bara aliibuka mfungaji bora akiwa na mabao saba akifuatiwa na mshambuliaji mwenzake Andrew Simchimba ambaye alifunga mabao sita sawa na Yoseif  Tesfai wa Eritrea.

Tanzania Bara ilifuzu fainali baada ya kuifunga Sudan kwa mabao 2-1 na Kenya ikaifunga Eritrea kwa bao 1-0.
Mpaka kutinga fainali Tanzania Bara ilifunga mabao 17 na imefunga mabao matano tu, mawili katika hatua ya makundi, mawili robo fainali na moja nusu fainali.
Mashindano ya CECAFA U20 yalianza kutimua vumbi Agosti 22, Tanzania bara ikiwa katika Kundi B pamoja na timu za Ethiopia, Zanzibar na Kenya na kundi A lilikuwa na timu za Uganda, Sudan, Sudan Kusini na Eritrea.

No comments:

Post a Comment