Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, April 24, 2018

TANZANIA PRISONS YAANZA VEMA KUTETEA UBINGWA WA MUUNGANO


MABINGWA watetezi wa kombe la Muungano kwa upande wa wanawake, timu ya Tanzania Prisons imeanza vema kutetea ubingwa wao baada ya kuifunga JKT kwa seti 3-0 katika mchezo uliochezwa jana katika viwanja vya Ziwani, Zanzibar.
Akizungumza kwa njia ya simu toka Zanzibar, nahodha wa timu hiyo Hellen Richard alisema wanashukuru kwa kupata ushindi huo kwani JKT ni moja ya timu ambayo walikuwa wanaiogopa.
“Tunashukuru kupata ushindi katika mchezo wa kwanza kwani ni mwanzo mzuri wa kutetea ubingwa ukizingatia JKT ni timu nzuri,” alisema Hellen
Kwa upande wa timu za wanaume, Faru imeshinda michezo yake miwili ambapo iliifunga Nyuki ya Zanzibar kwa seti 3-1 na kuifunga Mafunzo kwa seti 3-2.
Pentagone imecheza michezo miwili ikashinda mchezo mmoja na kupoteza mmoja ambapo iliifunga Nyuki kwa seti 3-1 na kufungwa na Polisi kwa seti 3-2 pia Polisi ikaifunga JKT kwa seti 3-0, ikaifunga Mafunzo seti 3-2 na kuifunga Nyuki seti 3-0.
Kwa upande wa wanawake JKT baada ya kufungwa na Tanzania Prisons iliifunga Polisi ya Zanzibar kwa seti 3-0.
Timu zinazoshiriki kwa upande wa wanaume ni Polisi, Nyuki na Mafunzo za Zanzibar, JKT, Faru na Pentagone za Tanzania Bara na kwa upande wa wanawake ni Polisi Zanzibar, JKT na Tanzania Prisons za Bara.
Kwa upande wa wanaume bingwa mtetezi Jeshi Stars hajashiriki msimu huu hivyo kombe haki sasa halina mwenyewe.

No comments:

Post a Comment