Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, April 24, 2018

SERENGETI BOYS UWANJANI KESHO KUCHEZA NA KENYA NUSU FAINALI CECAFA


TIMU ya Taifa ya Vijana U-17, Serengeti Boys, kesho inatarajia kutupa karata yake muhimu kwenye mchezo wa nusu fainali wa mashindano ya CECAFA dhidi ya Kenya.
Mchezo huo utachezwa saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Muyinga nchini Burundi.
Serengeti Boys imefuzu nusu fainali baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda kwenye mchezo wa kwanza na kuifunga Sudan kwa mabao 6-0 kwenye mchezo wa mwisho wa makundi
Akizungumza kocha wa Serengeti boys, Oscar Mirambo alisema mchezo dhidi ya Kenya utakuwa wa ushindani lakini kutokana na maandalizi waliyofanya na ari waliyonayo wachezaji watashinda.
“Tumefanya maandalizi ya kutosha, tunaamini tutafuzu fainali na ni nia yetu kushinda na kurudi na ubingwa huu,” alisema Oscar.
Wakati huo huo timu ya Taifa ya Vijana waliochini ya umri wa miaka
20, Ngorongoro Heroes imerejea nchini leo ikitokea nchini DR Congo kwenye mchezo wa marudiano wa kufuzu fainali za Africa za Vijana U-20 dhidi ya DR Congo ilishinda kwa penalti 6-5 baada ya suluhu katika dakika 90 za mchezo.
Baada ya kurudi wachezaji wote wamepewa mapumziko ya siku tatu na wakirejea wataendelea na program ya kocha mkuu Ammy Ninje kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa raundi ya pili dhidi ya Mali utakaochezwa mwezi ujao mchezo ambapo wataanzia nyumbani.

No comments:

Post a Comment