Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, April 22, 2018

NGORONGORO HEROES NA SERENGETI BOYS KARATA MUHIMU LEO


TIMU za Taifa za Soka za Vijana, zilizochini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys na U-20, Ngorongoro Heroes leo zinatarajiwa kushuka viwanjani kucheza michezo ya kimataifa.
Ngorongoro heroes itakuwa nchini DR Congo kwenye mchezo wa marudiano wa kutafuta kufuzu fainali za Afrika baada ya mchezo wa awali kutoka suluhu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kocha wa Ngorongoro Heroes’ Ammy Ninje  wamejiandaa vema kwa mchezo huo na wachezai wameahidi kucheza kufa ama kupona ili waweze kusonga mbele
"DRC ni timu ya kawaida kwani kama ni bora kuliko Ngorongoro wangepata ushindi katika mchezo wa kwanza uliochezwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, hivyo wasubiri kipigo katika mchezo  wa kesho (leo) ," alisema Ninje. 
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ndio imegharamia usafiri  kwa timu ya Ngorongoro ambayo iliondoka ikiwa na wachezaji 21 na benchi la ufundi ni watu saba
Nayo timu ya Vijana waliochini ya miaka 17, Serengeti boys inatarajia kucheza mchezo wake wa mwisho wa mashindano ya Cecafa katika hatua ya makundi  dhidi ya Sudan katika mkoa wa Gitega kuanzia saa 9:00 kwa saa za Burundi
Serengeti boys ambayo ilikuwa katika kundi moja na Zanzibar ambayo iliondolewa kwenye mashindano kwa madai ya kupeleka wachezaji ambao wamezidi umri inahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu nusu fainali.
Akizungumza jana Kocha wa timu hiyo Oscar Mirambo  alisema Serengeti boys ipo tayari kuhakikisha inaondoka na ushindi ili ifuzu nusu fainali na wana ari kubwa hivyo wanatarajia kushinda mchezo huo.
“Mchezo na Sudan ni muhimu kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri kwani ni mchezo wa mwisho katika hatua ya makundi,” alisema Oscar
Nusu fainali zitachezwa Aprili 24  na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu utachezwa fainali zitachezwa Aprili 28katika Uwanja wa Ngozi.
Mashindano ya CECAFA U-17 yatashirikisha timu saba ambazo ni Uganda, Sudan, Burundi, Kenya, Somalia na Ethiopia na Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment