Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, December 24, 2017

SIMBA YAMTUPIA VIRAGO OMOG

KLABU ya Simba imetangaza kuachana na kocha wao Joseph Omog kufuatia matokeo mabaya kwenye mchezo wa hatua ya pili ya kombe la Shirikisho la Azam Sports hapo jana.
 Hii hapa taarifa ya klabu hiyo;

Simba Sports Club
Dar es salaam
23/12/2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
_____________________________________
Klabu ya Simba na kocha wake mkuu Joseph Omog, wameamua kwa pamoja kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano maalum yanayozingatia maslahi ya pande zote mbili.
Klabu inamshukuru kocha Omog na inamtakia kila la kheri kwenye maisha yake nje ya Simba.
Kwa wakati huu Timu yetu itakuwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma na itaendelea na mazoezi kesho,na kupumzika siku ya Jumatatu kwa mapumziko ya sikukuu ya Christmas na itaingia kambini Jumanne kabla ya safari ya Mtwara,ambapo tutacheza na Timu ya Ndanda kwenye mchezo wa Ligi kuu wiki ijayo.
Pia kwa niaba ya uongozi, benchi la ufundi na wachezaji.tutumie nafasi hii kuwaomba radhi sana Wanachama na washabiki wetu kwa matokeo ya jana, sote tumeumia ila ndio mchezo wa mpira ulivyo, na tuwaombe muwe watulivu katika kipindi hiki ili tufikie malengo yetu.
Mwisho
klabu inawatakia nyote Sikukuu njema ya Noeli na mapumziko mema ya wikiendi.
IMETOLEWA NA….
Haji S MANARA
Mkuu wa Habari Simba Sc
SIMBA NGUVU MOJA

No comments:

Post a Comment