Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, December 3, 2017

SIMBA YABARIKI RASMI MO KUPEWA TIMU, AAHIDI MAKUBWA


KLABU ya Simba leo imeandika historia katika soka la Tanzania baada ya kukubali na kuingia rasmi katika mfumo wa hisa baada ya mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ kutangazwa mshindi wa zabuni ya kuweza kwa dau la Sh. Bilioni 20.
Akizungumza wakati akitangaza mchakato wa Jaji Mstaafu Thomas Mihayo alisema kuwa Mo ndiye mwekezaji pekee aliyejitokeza kuomba zabuni hiyo baada ya kutangazwa na kukidhi vigezo vyote vilivyowekwa.
“Mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ amepita katika mchakato wa awali wa uwekezaji wa klabu ya Simba kwa kukubaliwa kuwekeza Sh. Bilioni 20 kwani alikuwa mwombaji pekee aliyetuma maombi katika kamati yetu na ndiye mshindi wa tenda kwani ametimiza vigezo vyote,”.
“Tumejiridhisha kupitia Kamati Maalumu ya kutathimini Zabuni, lakini pia tunaangalia jinsi gani ataweza kulipa madeni ya klabu yaliyopo sasa, kodi zinazodaiwa na TRA na hatima ya michezo mingine kwani majadiliano zaidi yatafanyika baada ya mkutano wa leo (jana),” alisema Jaji Mstaafu Mihayo
Jaji Mihayo alieleza kuwa mwekezaji huyo atakuwa akiweka wazi mipango yote ya klabu ikiwemo kusajili wachezaji, kuajiri benchi la ufundi, kutengeneza viwanja vya mazoezi, gym, hosteli ya wachezaji, kuanzisha akamemi, bwawa la kuogelea na jengo la ofisi za klabu.
Pia alisema mwekezaji ameeleza jinsi ya kuwa na vyanzo vya mapato kwa klabu ikiwemo mapato ya getini, kodi za majengo, riba za fedha zitakazokuwa benki, uuzaji wa jezi, kofia na mengineyo.
Akizungumza baada ya kutangazwa Mo aliweka wazi ahadi kumi ambazo atatekeleza kuwa ni Kujenga viwanja viwili bora ambavyo vitakuwa na nyasi asilia na nyasi bandia, Kujenga hosteli ya wachezaji na benchi la ufundi yenye vyumba 35
Kujenga mgahawa kwa ajili ya wachezaji, kujenga gym na bwawa la kuogelea kwa ajili ya wachezaji, kujenga kituo cha kulea vijana chini ya umri wa miaka 14, 16, 18
Kurejesha Simba katika historia ya kimataifa, kutenga Sh. milioni 500 kwa ajili ya benchi la ufundi na Sh. bilioni moja kwa ajili ya usajili wa wachezaji kila msimu.
Kutengeneza brand ya Simba pamoja na vifaa vya klabu kama jezi, kofia, wachezaji kujituma na kutambua thamani ya klabu ya Simba na kushindana na timu kubwa Afrika.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Utalii Dk. Hamis Kigwangala na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Michael Wambura.

Awali, klabu hiyo ilisema mwekezaji atamiliki asilimia 50 ya hisa huku asilimia 10 zikitarajia kugawiwa kwa wanachama waliopo sasa na nyingine 40 kuuzwa kwa wadau wengine.