Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, November 4, 2017

YANGA YABANWA NA SINGIDA UNITED, ZAGAWANA POINTI



MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya soka Bara, Yanga wameshindwa kutamba ugenini kwenye Uwanja wa Namfua Singida dhidi ya Singida United baada ya kulazimishwa suluhu.
Yanga iliyokuwa na pointi 16 sasa imefikisha pointi 17 huku Singida United ikifikisha pointi 14 kwenye msimamo wa ligi ambao ulitarajiwa kubadilika baada ya matokeo ya Azam na Ruvu Shooting zilizotarajiwa kuchezwa usiku.
Wenyeji Singida United walitawala mpira kipindi cha kwanza na cha pili na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga ingawa ilishindwa kuzitumia kwa vipindi tofauti.
Safu ya kiungo ya Singida ilifanya vizuri kwa kutengeneza nafasi na mashambulizi ila washambuliaji walishindwa kufunga.
Upande wa Yanga, nafasi ya kiungo ilizidiwa na kushindwa kutengeneza nafasi za kufunga.
Kipindi cha kwanza kilimalizika Singida ikiongoza kwa mashambulizi mengi na hata kipindi cha pili bado walikuwa bora zaidi ya Yanga walioonekana kuzidiwa karibu muda mwingi.
Tafwadzwa Kutinyu alipata nafasi ya kufunga katika dakika ya  17 na 43 na kushindwa kutumia baada ya kipa wa Yanga, Youthe Rostand kuzipangua. Pia, Deus Kaseke na Danny Usengimana walikuwa wakipata nafasi na kushindwa kuzitumia.
Kwa upande wa Yanga, Geofrey Mwashiuya alipata nafasi akashindwa kuitumia.
Timu zote mbili zilifanya mabadiliko Singida ilimtoa Kaseke na kuingia Nhivi Simbarashe, Usengimana alitoka na kuingia Atupele Green, Yanga iliwatoa Mwashiuya na kuingia Emmanuel Martin na Raphael Daud aliingia kuchukua nafasi ya Pato Ngonyani lakini bado hakuna timu iliyopata ushindi.

Mechi nyingine zilizochezwa jana ni Mtibwa Sugar dhidi ya Ndanda zilizotoka suluhu matokeo kama hayo yalipatikana katika mechi ya Njombe Mji dhidi ya Mbao huku Kagera Sugar ikitoka sare ya bao 1-1 na Tanzania Prisons.

No comments:

Post a Comment