Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, November 4, 2017

TANZANIA YANG'ARA SOKA LA UFUKWENI AFRIKA

LIGI YA VYUO YA SOKA LA UFUKWENI YANUKIA
TANZANIA imeng’ara katika soka la ufukweni baada ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuitangaza ni ya 12 katika viwango vya mchezo huo katika Bara la Afrika.
Akizungumza Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas alisema Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limetoa viwango hivyo na Tanzania inashika nafasi ya 86 duniani na Afrika 12.
“Tanzania imeng’ara kwa mujibu wa viwango vilivyotangazwa juzi nchi za Senegal, Nigeria, Misri, Morocco, Madagascar, Ivory Coast, Ghana, Libya, Msumbiji, Cape Verde na Kenya ndizo zilizo juu ya Tanzania,” alisema Lucas.
Taarifa imekuja huku Tanzania ikiwa bado haijawahi kuwa na ligi ya mchezo huo zaidi ya ligi inayohusisha timu za taasisi za Elimu ya juu mkoa wa Dar es Salaam na Pwani pekee inayotarajiwa kuanza Novemba 9 katika Uwanja wa Karume Dar es Salaam. 
Mbali na ligi hiyo ya soka la ufukweni Tanzania imeshiriki mashindano ya kimataifa ya Afrika mara mbili, ambayo ndio imeipaisha katika viwango hivyo vya ubora.




No comments:

Post a Comment