Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, November 5, 2017

SIMBA YARUDI KILELENI, LIPULI YATOKA SARE NA MWADUI FC

SIMBA imefanikiwa kurejea kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifunga Mbeya City bao 1-0 katika uliochezwa kwenye  Uwanja wa Sokoine, Mbeya
Iliichukua Simba dakika saba kupata bao lililofungwa na Shiza Kichuya  baada ya kupokea mpira uliopigwa na Jonas Mkude ambaye alipokea pasi kutoka kwa Haruna Niyonzima aliyepiga mpira wa adhabu ndogo.
Katika kipindi cha kwanza Simba ilitawala mchezo na kufanikiwa kuliandama lango la Mbeya City huku dakika ya 43 Erasto Nyoni akikosa bao la wazi na kumaliza dakika 45 wakiwa na bao hiyo moja.
Kipindi cha pili Mbeya City walianza mchezo kwa kasi na kuliandama lango la Simba ambao walicheza mchezo wa kujihami muda mwingi lakini umakini wa kipa Aishi Manura walijikuta mipira ikiishia mikoni mwake.
Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi tisa na kupanda kileleni ikiizidi kwa wastani wa mabao Azam yenye pointi 19 pia na Yanga wakishika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 18 sawa na Mtibwa Sugar baada ya juzi kutoka sare.
Simba itasalia Mbeya hadi Novemba 18 itakapocheza na Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu na Jumamosi inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na Kyela kombaini kwenye Uwanja wa Mwakangale kabla ya kuivaa Prisons.
Kichuya amefikisha mabao matano (5) kwenye ligi sawa na Ibrahim Ajib wa Yanga huku akiwa anaziwa na Mohamed Rashid wa Tanzania Prisons mwenye mabao sita na Emanuel Okwi wa Simba anaeongoza akiwa na mabao nane.
Simba imeshinda mechi ya tatu kati ya tano ilizokutana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, kabla ya mchezo wa leo, Simba ilikuwa imeshinda mechi mbili kati nne, mchezo mmoja walitoka sare na mwingine walipoteza.
Mbeya City imepoteza mchezo wa pili kati ya mechi tano walizocheza kwenye uwanja wa Sokoine. Mchezo mwingine waliopoteza kwenye uwanja wa Sokoine ilikuwa dhidi ya Ndanda.
Kikosi cha Simba kilikuwa Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, James Kotei, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim dk 88, Muzamil Yassin/Laudit Mavugo dk 78, John Bocco, Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima /Said Ndemla dk55.
Kikosi cha Mbeya City kilikuwa ni Fikirini Bakari, Erick Kyaruzi, Hassan Mwasapili, Ally Lundenga, Sankan Mkandawile, Babu Ally, Mrisho Ngassa, Mohammed Samatta, Mohammed Mkopi/Victor Hangaya dk 82, Omary Ramadhani/Iddi Nado dk 64 na Eliud Ambokile. 
Katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Samora Iringa wenyeji Lipuli FC wametoka sare ya bao 1-1 na Mwadui FC
Wenyeji Lipuli FC  walipata bao dakika ya 48 lililofungwa na Asante Kwasi kwa penalti lakini Mwadui FC wakasawazisha dakika ya 70 bao lililofungwa na Abdallah Seseme .

No comments:

Post a Comment