Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, October 21, 2017

MIAKA 20 YA MALTCHOICE YAWAKUSANYA MASTAA KIBAO, DAR ES SALAAM








SERIKALI imeitaka Kampuni ya Maltchoice Tanzania kupunguza bei ya kulipia king’amuzi kwa mwezi ili iwe rafiki kwa wateja na kuongeza watumiaji.
Hayo yalisemwa jana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu katika sherehe ya kutimiza miaka 20 ya kutoa huduma nchini Tanzania iliyofanyika Dar es Salaam.
“Niwapongeze kwa kufikisha mihongo miwili ya kutoa huduma, mimi ni mtumiaji wa king’amuzi chenu na napenda kuangalia vipindi vya Eva na Maisha Magic Bongo kwani inasaidia kupumzisha akili baada ya kuchoka,”  alisema

“Pia niwapongeze kwa kuinua vipaji vya wasanii na wanamichezo hasa Simbu ambaye mmewekeza sh. milioni 300 kwa sasa anafanya vizuri katika riadha lakini muangalie namna ya kupunguza bei zenu ili ziwe rafiki kwa watumiaji,” alisema Samia.
Pia Samia aliwataka Maltchoice kuendelea kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwalipa wafanyakazi vizuri na kulipa kodi za serikali kwa wakati serikali imeweka mipango thabiti ya kutoa ushirikiano kwa makampuni binafsi.
Awali akizungumza, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe alisema Maltchoice wamekuwa mfano wa kuigwa kwani wamekuwa wakitoa huduma bora  na wameshiriki kuinua michezo.
“Kila mtu ameona mchango wa Maltchoice na wanajali ubora na hivi karibuni walishiriki tamasha la Jamfest lililofanyika nchini Uganda na kikubwa zaidi wamfadhili, Felix Simbu ambaye anafanya vizuri katika riadha kimataifa na wamenidokeza 2020 wanatamani kuona wimbo wa Taifa ukiimbwa katika mashindano ya Olympiki,” alisema Dk. Mwakyembe.
Awali akieleza historia Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande, alisema walianza kufanya kazi Tanzania 1997 ikiwa na wafanyakazi saba pekee na ilikuwa ikifanya kazi Dar es Salaam peke yake lakini sasa wapo mikoa yote.
“Tulianza kufanyakazi tukiwa na wafanyakazi saba pekee na ilikuwa tabu kutoa huduma mikoa ukizingatia pia teknolojia ilikuwa haijakuwa kama sasa,”
“Ilichukua siku mbili hadi tatu kufunga dishi lakini jinsi teknolojia ilivyokuwa kazi hiyo inafanyika katika dakika kadhaa tu hata kufikia wateja mikoa ilikuwa shida na wateja wa mikoani ili kulipia ilibidi waende benki halafu wanatuma fax ili waweze kuunganishiwa huduma,” alisema Chande.

Pia Chande alisema changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni pale wanapotaka kubadilisha madishi baadhi ya wateja wanakataa wakidai wanalotumia halina tatizo hivyo wanawapa elimu na hatimaye wanakubaliana.

No comments:

Post a Comment