Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, October 18, 2017

MBAO FC WAKABIDHIWA BASI LAO NA GF TRUCKS


NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amesema msimu huu wamepania kuhakikisha ubingwa wa Ligi Kuu unaondoka Dar es Salaam.
Angelina ambaye ni mbunge wa Ilemela aliyasema hayo leo wakati akipokea basi kutoka Kampuni ya GF Trucks ambao ni wadhamini wa Mbao FC.
“Niwashukuru GF Trucks kwani msaada wao umekuja wakati muafaka na utachochea malengo yetu ya kuondoa  ubingwa wa ligi kuu kwa timu za Dar es Salaam,” alisema
“Tuache usimba na uyanga ndio mpira utakuwa na mnakumbuka Mbao FC wachezaji wengi waliondoka tukabaki na wachezaji nane tu lakini tumeibua vipaji vingine na vinafanya maajabu,” aliongeza Angelina Mabula.
Pia Angelina Mabula alisema yeye ni mshabiki wa Yanga lakini linapokuja swala linalohusu timu za nyumbani hasa mkoa wa Mwanza anakuwa upande wa Mbao ndio maana waliweza kuzizuia Simba na Yanga zisiondoke na pointi tatu katika michezo yao.
Naye Mkurugenzi wa GF Trucks Alijawah Karmali alisema anashukuru kutimiza moja ya makubaliano yao waliyoingia na Mbao Agosti 25 mwaka huu
“Hatua hii imetengeneza uhusiano mzuri kwa kampuni na wakazi wa kanda ya ziwa katika kukuza masoko ya bidhaa zake na kuchangia maendeleo ya jamii kwa ujumla,” alisema Karmali.
GF Trucks iliingia mkataba na Mbao FC wenye thamani y ash 140,000,000 ambapo sh milioni 70,000,000 zimenunulia basi lenye uwezo wa kubeba watu 33 ambalo lilikabidhiwa jana.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Njashi na wajumbe wa bodi ya Mbao FC, Amoni Asabuki na Masalida Njashi pamoja wafanyakazi wa GF Trucks &Equipments.