Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, August 2, 2017

UCHAGUZI MKUU TAFCA AGOSTI 10, 2017

Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA utafanyika Agosti 10, mwaka huu mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi), Ramadhani Mambosasa ametangaza orodha ya majina sita ya mwisho ya wagombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo.
Kwa mujibu Mambosasa, wagombea hao kwa sasa hawana budi kuendelea na kampeni hadi Agosti 9, mwaka huu.
Waliopitishwa katika orodha ya mwisho kuwania nafasi mbalimbali za uongozi - ngazi ya taifa ni pamoja na Kidao Wilfred, Lister Manyara, Michael Bundala, Dismas Haonga, Jamhuri Kihwelo, George Komba, Samuel Moja na Maka Mwalwasi na Mohammed Tajdin.
Nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

No comments:

Post a Comment