Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, July 8, 2017

ZENA CHANDE, SOMOE NG'ITU, AMINA KARUMA NA ROSE KISIWA WAULA TWFA







MHARIRI Msaidizi wa habari za michezo wa gazeti hili, Zena Chande amechaguliwa kuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Shirikisho la Soka (TFF) katika uchaguzi wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), ulifanyika leo Dar es Salaam.
Zena ambae alikuwa anatetea nafasi hiyo alipata kura 44 kati ya kura 52 zilizopigwa huku mpinzani wake Salma Wajeso akiambulia kura nane.
Katika nafasi ya Mwenyekiti, Amina Karuma alifanikiwa kutetea kiti chake kwa kura 47 huku kura tano zilimkataa kwani alikuwa mgombea pekee na Rose Kisiwa alitetea nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti kwa kura 46 na kura sita zikimkataa
Naye mwandishi mwandamizi wa Nipashe, Somoe Ng’itu alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu kwa kura 49 huku kura mbili zikimkataa na katibu msaidizi alichaguliwa Theresia Mung’ong’o kwa kura 44 na kura nane zikamkataa.
Nafasi ya mhazini alichaguliwa Hilda Masanche kwa kupata kura 25 huku kura 24 zikimkataa na kura tatu zikaharika na nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ilikosa watu baada ya wagombea kushindwa kufikia nusu ya kura za wajumbe.
Wajumbe wa kamati ya utendaji ilihitaji watu wanne na wagombea walikuwa wanne ambao ni Triphonia Temba kura 15, Chichi Mwidege kura 12, Mwamvita Kiyogoma kura 9 na Jasmine Soudy  kura saba.
Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo hayo Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Msomi Wakili George Mushumba, alisema wagombea hao walihitaji kupata kura zaidi ya nusu ya wapiga kura ambao ilikuwa ni 52 ili wawe wajumbe.
“Najua katiba inaruhusu kuteua wajumbe wawili lakini hao waliogombea wameshindwa hivyo uongozi uliochaguliwa utaona namna inayofaa ili waweze kuendelea na kazi zao za kuendeleza soka la wanawake,” alisema Mushumba.
Pia Mushumba aliwashukuru wagombea na wajumbe wa mkutano huo kwa ushirikiano walioonesha kwa kamati kipindi chote kuanza kwa mchakato wa uchaguzi na kuwataka kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuleta maendeleo.
Naye Mwenyekiti wa TWFA, Amina Karuma aliwashukuru wajumbe kwa kuwarudisha madarakani kwa kishindo na kuishukuru kamati ya uchaaguzi kwa kazi nzuri waliyofanya kwa kusimamia uchaguzi.
“Bila ushirikiano na ninyi sisi hatuwezi kufanya chochote hivyo naomba tuendelee kushirikiana ili tuzidi kufanya mazuri zaidi ya hayo tuliyokwisha kufanya,” alisema Karuma.
Uchaguzi huo ulifanyika kwa amani na wajumbe walipiga kura mmoja mmoja kwenye chumba maalumu baada ya kila nafasi wagombea wake kujieleza.

No comments:

Post a Comment