Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, July 23, 2017

VIJANA RANGERS YAFUZU ROBO FAINALI NDONDO CUP


TIMU ya Vijana Rangers imefuzu robo fainali ya mashindano ya Ndondo baada ya kuifunga Temeke Squad bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Kinesi Urafiki, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ambao ulijaa wachezaji chipukizi tofauti na timu zingine ambazo zimesheheni wachezaji mastaa wa Ligi Kuu, Vijana walipata bao dakika ya 28 lililofungwa na Yahaya Mbegu kwa mpira wa adhabu kubwa nje ya eneo la penalti.

Baada ya bao hilo kila timu ilijaribu kushambulia lango la mpinzani lakini umahiri wa makipa ulifanya dakika 90 zikamilike ubao ukisomeka Vijana 1 na Temeke 0.

Katika mchezo huo mshambuliaji wa Vijana Rangers, Yahaya Mbegu alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo na kupewa sh. 50,000,  Vijana Rangers nayo ikaondoka n ash. 150,000 na Temeke Squad 100,000 kutoka kwa kampuni ya mcheza Tanzania.

Kwa matokeo hayo Vijana imeungana na Goms United, Mlalakuwa Rangers, Mpakani Kombaini kufuzu nusu fainali na leo kutakuwa na mchezo kati ya Kibada One na Kigogo.