Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, July 15, 2017

TAIFA STARS YATOKA SARE NYUMBANI NA RWANDA

 
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars  imeshindwa kufurukuta kwenye uwanja wake wa nyumbani, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wageni wao Rwanda, 'Amavubi'.
Mchezo huo wa kuwania kufuzu fainali zijazo za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani, ulishuhudia Stars ikicheza mbele ya Watanzania lukuki ikishindwa kupata ushindi.
Rwanda, Amavubi ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Dominique Nshuti kunako dakika ya 17 kipindi cha kwanza, mlinzi Shomari Kapombe aliumia baada ya kuchezewa rafu mbaya na kutolewa nje.
Stars ilisawazisha bao katika dakika ya 34 kipindi hicho hicho cha kwanza kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na nahodha wake Himid Mao Mkami 'Ninja' baada ya beki wa kushoto Gardiel Michael kuangushwa.
Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa sare, kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kila timu zilishambuliana kwa zamu lakini hadi mwisho miamba hiyo ya Afrika mashariki ilimaliza kwa sare, kwa matokeo hayo, Stars imejiweka shakani kutinga hatua inayofuata kwani inahitaji sare ya kufungana zaidi ya bao moja ama kushinda wakati Rwanda inahitaji sare tasa tu ili kusonga mbele

No comments:

Post a Comment