Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, July 22, 2017

TAIFA STARS KATIKA KIBARUA KINGINE KIGALI LEO

 
TIMU ya soka ya Taifa Stars inashuka dimbani leo Jijini Kigali, Rwanda kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) dhidi ya Rwanda, Amavubi.
Taifa Stars inajitupa uwanjani ikiwa imeongezewa nguvu na mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva aliyeachwa wakati Stars ilipoondoka Dar es Salaam.
Mchezo huo ni wa marudiano baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Jumaosi iliyopita Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mchezo wa leo ni muhimu kwa Stars kwani inahitaji ushindi au sare ya mabao 2-2 isonge mbele na kucheza ama na Uganda au Sudan Kusini ambazo zinarudiana pia.
Katika mchezo wa awali uliofanyika Sudan Kusini, zilitoka suluhu. Sare ya 1-1 inaiweka Taifa Stars katika wakati mgumu kwani zikitoka suluhu leo au kufungana au ikafungwa, itatolewa.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga anatakiwa kupanga kikosi imara ambacho kitacheza kwa bidii na kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa leo.
Msuva aliyebaki kushughulikia mipango ya kujiunga na timu moja ya Morocco, anatarajiwa kuiongezea Stars nguvu na hivyo kutoa matumaini ya ushindi.
Hata hivyo, Taifa Stars inatakiwa kuacha ndoto za kutoka sare kwani kufanya hivyo kutaikosesha nafasi ya kuelekea kufuzu kwa mara ya pili kwa fainali hizo baada ya kucheza kwa mara ya kwanza mwaka 2009 Ivory Coast.
Katika fainali hizo, Tanzania ilipangwa Kundi A na Senegal, wenyeji Ivory Coast, Zambia na Senegal. Ilimaliza ikiwa ya tatu kwa kuwa na pointi nne.
Zambia na Senegal zilifuzu kwa hatua ya robo fainali baada ya kumaliza nafasi ya kwanza na pili kila moja ikiwa na pointi tano zikitofautiana mabao.
Katika kikosi cha sasa cha Stars, ni Erasto Nyoni pekee alikuwemo katika kile kilichocheza fainali hizo mwaka 2009 ambacho kilishinda 1-0 dhidi ya Ivory Coast, kilifungwa 1-0 na Senegal na kutoka sare ya 1-1 na Zambia.
Baada ya mchezo wa Mwanza, Stars ilitua mapema Kigali, Rwanda kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa ili iweze kupata matokeo mazuri katika mchezo wa leo.
Bado Taifa Stars ina kazi ngumu kwani kikosi hicho hakijaelewana vizuri na Rwanda sio timu ya kubeza kwani wako vizuri na wanacheza kwa kuelewana.
Kocha Mayanga alisema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo na kitapambana `kiume kuibuka na ushindi katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Amahoro.
Naye nahodha wa timu hiyo, Himid Mao alikaririwa akisema kuwa atahakikisha timu yake inacheza vizuri kushinda.
Waamuzi wa mchezo
Mchezo utachezeshwa na Brian Nsubuga Miiro huku akisaidiwa na Ronald Katenya na Dick Okello. Wa akiba ni Chelanget Ali Sabila. Kamishna wa mchezo atakuwa Ali Mohamed Ahmed kutoka Somalia.
WAGANDA KUCHEZESHA MECHI YA STARS NA RWANDA LEO A+ A- Print Email SHIRIKISHO la mpira wa miguu Afrika (CAF), limewateua waamuzi wa Uganda kuchezesha mchezo wa marudiano kati ya timu ya taifa ya Rwanda “Amavubi” na Taifa Stars ya Tanzania kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za ndani (CHAN). Stars na Rwanda zinarudiana leo Jumamosi kwenye uwanja wa Nyamilambo mjini Kigali baada ya kutoka sare ya bao 1-1 jijini Mwanza wiki iliyopita na timu inayoshinda ndio itakayofanikiwa kusonga mbele. Mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua utachezwa saa 10:00 jioni kwa saa za Rwanda ambazo ni sawa na 9:00 alasiri kwa saa za Tanzania na utachezeshwa na Brian Nsubuga Miilo ambaye ni raia wa Uganda atakayepuliza kipyenga cha kati. Atasaidiana na Ronald Katenya (Line 1), pamoja na Dick Okello (Line 2), wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Cheleneti Ally Sabila hukukamishina wa mchezo atakuwa ni Ally Ahmed Mohammed kutoka Somalia. Stars ina matumaini ya kusonga mbele kutokana na rekodi yake ambapo hadi sasa imecheza jumla ya mechi 10 za kimataifa, imeshinda mechi nne, sare tano na kupoteza mchezo mmoja wa nusu fainali ya michuano ya COSAFA.

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2017/07/waganda-kuchezesha-mechi-ya-stars-na.html#more
Copyright © saluti5

No comments:

Post a Comment