Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 28, 2017

SHAFIIH DAUDA ATANGAZA KUJITOA KWENYE UCHAGUZI TFF Image result for shaffih dauda images
MGOMBEA wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania kutoka kanda ya Dar es Salaam, Shaffih Dauda amejitoa
Akizungumza kupitia kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo cha Televisheni ya Clouds ambapo pia yeye ni mtangazaji Shaffih alisema amefikia hatua hiyo baada ya kuona mbinu na siasa chafu zinazoendeshwa juu yake.
“Mimi ni mfanyakazi wa Clouds Media Group nilikwenda Mwanza kwa ajili ya kazi. Hapa Clouds tumelelewa kufanya kazi kwa bidii kufikia malengo hivyo sitaki mambo yangu binafsi (kugombea uongozi TFF) kuharibu malengo ya mashindano ya Ndondo na taasisi yangu,” alisema Shaffih
“Nimeangaika kutengeneza jina langu kwa miaka mingi. Natangaza kujitoa rasmi kugombea, nitaendelea kuchangia kwenye maendeleo ya soka nikiwa sio kiongozi,” alisema Shaffih.
Pamoja na kuwa alikuwa anagombea ujumbe wa kamati ya Utendaji TFF pia ni mjumbe wa Mkutano Mkuu kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na Chama cha soka mkoa wa Ubungo (UFA) ni kiongozi pia.
Kauli ya Shaffih kujitoa imekuja ikiwa ni siku nne tangu akamatwe na Taasisi ya Kuzuia na  kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za rushwa pamoja na viongozi wengine wa soka kumi.
Hata hivyo kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inatarajiwa kukutana leo kwa ajili ya kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea wa nafasi mbalimbali wa uchaguzi wa TFF ambao wataanza kampeni Agosti 5.