Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, July 31, 2017

RAPHAEL DAUD ASAINI YANGA MIAKA MIWILI 
YANGA imefanikiwa kumsajili kiungo mshambuliaji Raphael Daudi kutoka Mbeya City kwa mkataba wa miaka miwili.
Akizungumza na mtandao huu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika alisema Raphael ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ usajili anakuwa mchezaji wa nane kusajiliwa na Yanga msimu huu.
“Tunafurahi kufanikiwa kukamilisha usajili wa Raphael Daudi kutoka Mbeya City ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili,”alisema.
Raphael anakuwa mchezaji wa nane kusajiliwa Yanga kwa msimu huu baada ya makipa Youth Rostand kutoka African Lyon, Ramadhan Kabwili, beki Abdallah Hajji kutoka Taifa Jang’ombe, viungo Pius Buswita kutoka Mbao FC, Papy Kabamba Tshishimbi kutoka Mbabane Swallows ya Swaziland, Hussein Akilimali huru na mshambuliaji Ibrahim Ajib kutoka Simba.
Raphael alikuwemo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichocheza michuano ya COSAFA na kutwaa medali ya Shaba baada ya ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Lesotho kufuatia sare ya 0-0 dakika 90 Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg.
Baada ya kusaini mkataba huo, Raphael amekwenda moja kwa moja kambini Morogoro kujiunga na wenzake kwa maandalizi ya msimu mpya.