Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, July 11, 2017

NDEMLA NA KABWILI WA SERENGETI BOYS WAONGEZWA TAIFA STARSKocha mku wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga ameendelea kukiboresha kikosi chake kwa kuwaongezea wachezaji wapya kuelekea mechi ya kufuzu michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani.
Kipa wa Serengeti Boys, Ramadhan Kabwili, kiungo wa Simba Said Ndemla na mshambuliaji wa Majimaji, Kelvin Sabato wamejumuishwa katika kikosi hicho ambacho kiliondoka jana kwenda Mwanza.
Wakati huo, wachezaji watatu wameachwa kutokana na kuwa majeruhi. Wachezaji hao ni kipa Beno Kakolanya, washambuliaji Shaban Idd na Mbaraka Yusuph.