Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 7, 2017

MTOTO BRADLEY SHABIKI WA SUNDERLAND AFARIKI LEO

 

Image may contain: 1 person, outdoor
Ujumbe wa wazazi wa Bradley Lowery ambaye alikuwa shabiki wa kutupwa wa Sunderland.
 Mtoto huyo mwenye miaka 6 aliyegusa maisha ya watu wengi amefariki Dunia leo baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
Mshabiki huyo wa kutupwa wa Sunderland alikua akisumbuliwa na Ugonjwa wa Saratani tangu akiwa na miezi 18.
_Kifo cha Bradley kimethibitishwa na Wazazi wake kwenye mitandao ya Kijamii kwa kuandika ujumbe ufuatao
 " Kijana wetu jasiri amesafiri na Malaika leo, 07/07/17, saa 13:35, akiwa kwenye mikono ya wazazi wake, huku ndugu zake wakiwa wamemzunguka. 💔💔💔
Ni shujaa wetu. Amepambana vita kubwa sana lakini sasa amehitajika mahala pengine.
Hakuna maneno tutakayoweza kutumia yakatosha kuelezea jinsi mioyo yetu ilivyoumia.
Ahsanteni wote kwa ushirikiano mliouonyesha kwake mpaka aliposafiri safari yake ya mwisho.
Lala salama kijana wetu. Malaika wa Mungu wako pamoja nawe.💙"
#Rest in peace little brother!