Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 7, 2017

KWASI AJIWEKA SOKONI



 Image result for Asante Kwasi
ALIYEKUWA beki wa kati Mbao FC ya Mwanza Asante Kwasi amesema yuko tayari kutua timu yoyote ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao
Kauli ya Kwasi imekuja baada ya kumalizika kwa mkataba wake na Mbao FC ambao nao bado hawajaonesha nia ya kumwihitaji wala kuzungumza kuhusu mkataba mpya.
Akizungumza na gazeti hili Kwasi alisema yupo huru baada ya kumaliza mkataba wake na Mbao mpaka sasa bado hajafanya mazungumzo na timu yoyote.
“Nipo nyumbani Ghana, mkataba wangu na Mbao umeisha na bado sijafanya mazungumzo na timu yoyote. Mpira ni kazi yangu ikitokea timu tutakayokubaliana maslahi nitajiunga nayo haraka,” alisema Kwasi.
Naye Mwenyekiti wa timu hiyo Solly Zephania alikiri kutoendelea na beki huyo msimu ujao na kumtakia kila la kheri katika maisha yake ya soka.
“Msimu ujao hatutakuwa na Kwasi, mkataba wake umemalizika na tumekubaliana kwa pamoja kuwa hatutaendelea nae,” alisema Zephania.
Kwasi alitengeneza kombinesheni nzuri katika safu ya ulinzi imara na nahodha Yusuph Ndikumana ambayo iliyowasumbua washambuliaji wengi msimu uliopita lakini baada mkataba kumalizika uongozi ukaamua kumruhusu kutimka.

No comments:

Post a Comment