Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 12, 2017

KOTEI ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA

 
KIUNGO wa Simba, James Kotei amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo, na kusema amefurahi kubakia hivyo mashabiki wajiandae kufurahi
Akizungumza Kotei alisema ni wakati wake wa kupiga kazi ndani ya kikosi hicho.
“Nimefurahi kusaini mkataba mpya, hii ni timu ambayo mashabiki wake wana upendo, naamini viongozi wameona mchango wangu ndio sababu wamenipa mkataba, sasa huu ni wakati wa kuchapa kazi.
“Nimesaini mkataba wa miaka miwili, kutokana na furaha niliyonayo naahidi kuongeza juhudi ili kuhakikisha nafanya vizuri zaidi ya mwanzo,” alisema Kotei.
Kotei alimaliza mkataba wake wa miezi sita na Simba ambapo walishindwa kumpa mkataba mrefu kwa madai ya kutaka kujiridhisha kwanza na kiwango chake jambo ambalo amelithibitisha kwa vitendo baada ya kuwa msaada mkubwa kwa kipindi chote alichokuwepo ndani ya Simba.
Simba hawakuwa na haraka ya kumwongeza mkataba mpya mchezaji huyo hata baada ya kuwepo na taarifa za watani wao kuhitaji huduma ya Kotei.
Hivi karibuni Yanga walikuwa wanasaka saini ya mchezaji huyo lakini walishindwa kuipata kutokana na Kotei kuwa na msimamo wa kuipa nafasi ya kwanza Simba ambayo ni timu ya kwanza kumleta nchini.

No comments:

Post a Comment