Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 28, 2017

KIBADA ONE YAFUZU NUSU FAINALI NDONDO CUP 
TIMU ya     Kibada One imefuzu nusu fainali ya mashindano ya Ndondo kwa penati 4-2 baada ya matokeo ya sare ya kufungana 1-1 katika dakika 90 dhidi ya Vijana Rangers katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Kinesi Urafiki, Dar es Salaam.
Vijana ndio walianza kupata bao la kuongoza dakika ya kwanza likifungwa na Anuar Jabir kufuatia shambulizi kali la kushtukiza lililofanywa baada ya kuanzishwa kwa mpira.
Kibada One walisawazisha bao hilo dakika ya 41 kupitia kwa Selemani Mkonde baada ya mabeki wa Vijana kusimama wakidhani ameotea bao lililodumu hadi dakika 90 na kupigiana penalti
Akizungumza baada ya mchezo kumalizika Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Janury Makamba alisema soka la Tanzania linakabiliwa na changamoto nyingi huku akipongeza vijana kujumuika kuangalia mechi hizo.
“Changamoto kubwa ni kuendeleza soka la Tanzania, mpira unahitaji vitu vinne ili ufanikiwe ambavyo ni vipaji, pili miundo mbinu ya mchezo ambayo ni viwanja, akademi, tatu mifumo ya kuvumbua na kuendeleza vipaji na utawala bora katika michezo,” alisema Makamba.
Makamba alisema ameshuhudia mchezo mzuri sambao ulikuwa na ushindani na nguvu sawa ndio maana mshindi amepatikana kwa penalti.
Katika mchezo huo mchezaji wa Vijana Rangers Anwar Jabir alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi na kuzawadiwa sh 50,000 na timu yake ikaondoka n ash 100,000 huku Kibada One ikijichukulia sh 150,000 kutoka kwa Kampuni ya Mcheza Tanzania.