Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, June 1, 2017

WENGER AANZA MAWINDO YAKE



 The Soccer Saturday pundits have offered their advice to Arsene Wenger for the next two seasons
BAADA ya Arsene Wenger kuthibitisha kubaki Emirates inaelezwa kwamba amewaweka kwenye rada zake mshambuliaji wa AC Milan kutoka Colombia, Carlos Bacca (30), winga wa Leicester mzaliwa wa Algeria, Riyad Mahrez (26) na kiungo wa Monaco, Thomas Lemar (21).
Wenger inaelezwa anaruhusiwa kutumia pauni milioni 100 kwa ajili ya usajili, kiasi ambacho bado ni kidogo, ikilinganishwa na Manchester City ambao wamemwambia Pep Guardiola atumie hadi pauni milioni 250 kwa usajili. Liverpool na Man United nao wanajipanga kuvunja benki, Chelsea wakisema hawana nia ya kutapanya fedha.
Mlinzi wa Southampton, Virgil van Dijk (25) anapenda kujiunga Liverpool, wanaoelezwa kwamba wapo tayari kumchukua Mholanzi huyo kwa pauni milioni 50 hivi ili aimarishe kikosi chao tayari kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).
Mshambuliaji wa Ufaransa na Atletico Madrid, Antoine Griezmann (26) ameiambia klabu kwamba anataka kuondoka, lakini kifungu cha mkataba cha kumwezesha kuaga Madrid kinataka klabu chukuzi iweke mezani £87m, huku Manchester United wakihusishwa na kumtaka.
Kiungo wa Paris Saint-Germain (PSG) na Ufaransa, Blaise Matuidi (30) anasema kwamba hana uhakika iwapo atakuwa klabuni hapo msimu ujao, na hizi ni habari njema kwa United, kwani wamekuwa wakimtafuta kwa muda.
Jose Mourinho anataka Matuidi acheze sambamba na Andre Herrera na pengine awe mrithi wa Michael Carrick anayetarajia kuondoka Old Trafford baada ya mwaka mmoja. Pia Matuidi anaweza kujiungisha vyema na Mfaransa mwenzake, Paul Pogba huko mbele.
Mlinzi Mdachi wa Chelsea, Nathan Ake (22) anatarajiwa kuingia kwenye mazungumzo na klabu kuona iwapo atahitajika klabuni au aende kwa mkopo msimu ujao.
 Mshambuliaji Mnigeria wa Manchester City, Kelechi Iheanacho (20) anataka kubaki England japokuwa klabu wanaelekea hawampendi, na atakataa ofa kutoka kwa PSG ili asubiri wengine wa England. Man City, hata hivyo, hawangependa kumuuza kwa wapinzani wao katika EPL.
Kocha wa Newcastle, Rafael Benitez anataka kuungana tena na kipa wa zamani wa Liverpool, Pepe Reina na analenga kutoa pauni milioni nne kumchukua Mhispania mwenzake huyo kutoka klabu ya Napoli, Italia.
Marseille wa Ufaransa wanataka kumsajili winga wa Spurs, Moussa Sissoko wakati Chelsea wanamtaka kipa wa PSG, Mfaransa Alphonse Areola (24) ili achukue nafasi ya raia wa Bosnia, Asmir Begovic aliyejiunga na Bournemouth.

No comments:

Post a Comment