Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, June 15, 2017

TFF YAIGOMEA BMT YAOMBA KUKUTANA NAO MAPEMA ZAIDISHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema halitasitisha mchakato wa Uchaguzi Mkuu licha ya kupokea barua ya zuio kutoka Baraza la Michezo Tanzania (BMT)
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine alikiri kupokea barua ya BMT na kusema wamewaandikia kukutana nao mapema.
“Tunatarajia kukutana nao maana namini wanafanya hivi kwa sababu ya afya ya mpira wa miguu lakini hatutasimamisha uchaguzi kwa sababu utakuwa nje ya katiba,” alisema Selestine.
Selestine alisema katiba ya TFF inawakata uchaguzi kufanyika kabla ya Agosti kumalizika hivyo wakisitisha mchakato watakuwa wanakiuka katiba.
“Uchaguzi Mkuu wa TFF ni agenda moja tu katika mkutano huo hivyo ukisitisha mchakato wa uchaguzi unaweza kujikuta umefika mwakani bila uchaguzi kufanya pia kamati inayosimamia uchaguzi ipo kihalali kulingana na katiba ya TFF,” alisema Selestine.
Juni 13 Baraza la Michezo lilimwandikia barua kwa Katibu Mkuu wa TFF kutaka kusitishwa kwa uchaguzi wa viongozi wakuu wa TFF kwa sababu halijajulishwa kuwepo kwa uchaguzi huo.
Pia barua hiyo iliwataarifu TFF kuwa kamati ya nidhamu, rufaa na usuluhishi ya Baraza inataka kukutana na kamati ya itendaji ya TFF Julai Mosi saa nne asubuhi katika ofisi za baraza zilizopo Uwanja wa Taifa.
Lakini pia Selestine alisema wao wana katiba yao inayojitegemea na wanapaswa kuwasilisha BMT matokeo ya uchaguzi lakini siyo kuwajulisha juu ya mchakato wa uchaguzi.
Wakati huo huo, Mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF anayewakilisha kanda ya Tabora na Kigoma, Alhaji Ahmed Mgoyi ametangaza kutogombea nafasi yoyote katika uchaguzi ujao.
Alhaji Mgoyi amekuwa mjumbe wa Kamati ya utendaji kwa muda mrefu (2004-2017) kuanzia enzi za utawala wa Leodgar Tenga hadi sasa kwenye uongozi wa Jamal Malinzi.
Katika waraka wake aliotoa katika vyombo vya habari Alhaj Mgoyi alisema ameamua kwa ridhaa yake ili kutoa fursa kwa wengine kugombea na kuomba radhi kwa watu ambao hawakutarajia kuona akitoa uamuzi huo.