Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, June 15, 2017

Milioni 50, Gari Vyampeleka Ajibu Yanga


DEAL done! nyota wa Simba Ibrahim Ajibu amemalizana na Yanga kwa kusaini mkataba wa miaka miwili na kwamba ataitumikia klabu hiyo msimu ujao baada ya kutisha kwa misimu kadhaa akiwa na wekundu hao wa mtaa wa Msimbazi. Vuta nikuvute ya fundi huyo wa mpira na viongozi wake imechukua muda mrefu lakini mwisho wa siku vigogo hao wakakubali kushindwa kimya kimya ndipo viongozi wa Yanga walipotumia mwanya huo kumaliza biashara mapema mchana wa leo.
Ibrahim Ajibu
Ajibu amepewa pesa ya usajili Sh 50 milioni pamoja na gari ndogo ya kutembelea huku usajili huo ukifanywa kwa siri kubwa ili kukwepa ‘msala’ walioupata baada ya kumsajili beki wa kulia Hassan Ramadhan ‘Kessy’ akiwa hajamaliza mkataba wake msimu uliopita.
Mkataba wa Ajibu na Simba utamalizika mapema mwezi ujao na viongozi wa Yanga wamepanga kuweka hadharani kila kitu wakati huo huku sasa wakipambana kukanusha kila kitu kuhusiana na uhamisho huo.
Huu unakuwa usajili wa pili kwa Yanga baada ya jana kumalizana na beki wa kati wa Taifa Jang’ombe Abdallah Hajji.