Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, June 14, 2017

MAYANGA AITA 22 KWA AJILI YA COSAFA, KUINGIA KAMBINI JUMAPILI



WACHEZAJI wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta na Farid Mussa wameachwa katika kikosi kinachokwenda kushindana kuwania mashindano yanaandaliwa na Baraza la soka la nchi za Kusini mwa Afrika (COSAFA) nchini Afrika Kusini
Katika kikosi hicho Kocha Salum Mayanga ametangaza wachezaji 22 ambao watashiriki Kombe la Castle Cosafa nchini Afrika Kusini yanayotarajiwa kuanza Juni 25 na wataingia kambini Jumapili ya wiki hii.
Katika safu ya ushambuliaji Mayanga ameongeza , Stamil Mbonde, Elius Maguli ambao wanacheza soka Oman katika klabu ya Dhofar SC na kuwaacha Mbwana Samatta, Ibrahim Ajib na Abdulrahman Mussa.
Kadhalika katika nafasi ya viungo washambuliaji ameawaacha, Jonas Mkude, Salum Abobakar ‘Sure Boy’ na Farid Mussa na kumwongeza Rapahel Daudi kutoka Mbeya City ambaye atasaidiana na Mzamiru Yassin, Simon Msuva na Shizza Kichuya.
Akizungumza kocha Mayanga alisema anaamini kikosi hicho kitakwenda kutetea bendera ya Tanzania katika mashindano japo wanashiriki kama mwaliko.
“Nimelazimika kutumia wachezaji wengi wanaocheza ligi ya ndani kwani baada ya COSAFA Julai tutakuwa na mchezo wa kuwania kufuzu mashindano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani (CHAN) hivyo watakuwa wamepata maandalizi,” alisema Mayanga.
Kikosi hicho kinaundwa na makipa Aishi Manula  (Azam FC), Benno David Kakolanya  (Yanga) na Said Mohammed Said (Mtibwa Sugar).
Walinzi wa pembeni upande wa kulia ni Shomari Kapombe  (Azam FC) na Hassan Ramadhan ‘Kessy’ (Yanga) wakati upande wa kushoto wapo Gadiel Michael (Azam FC) na Amim Abdulkarim (Toto Africans).
Walinzi wa kati ni Erasto Nyoni  (Azam FC), Salim Abdallah (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons) wakati viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Salmin Hoza (Mbao FC).
Viungo washambulia ni Mzamiru Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga), Raphael Daudi (Mbeya City) na Shizza Kichuya (Simba).
Washambuliaji ni Thomas Emmanuel Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar), Stamili Mbonde, Elius Maguli (Dhofar SC) na Shabani Idd Chilunda (Azam FC).
Tanzania imepangwa kundi A ambako wapinzani wake ni Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe.
Tanzania itacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Malawi Juni 25 kabla ya kukutana na Angola Juni 27 na kumaliza hatua ya makundi Juni 29 kwa kucheza na Mauritius.
Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini, Namibia, Lesotho na Swaziland zitakuwa na mechi maalumu ya mtoano (play off) ili kuingia robo fainali ya mashindano haya ambayo yalianzishwa 1997  na yatashirikisha timu 14

No comments:

Post a Comment