Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, June 1, 2017

MAN UNITED KLABU TAJIRI ZAIDI DUNIANI



 Image result for MAN UNITED
WANAWEZA kuwa wamemaliza Ligi Kuu ya England (EPL) katika nafasi mbovu ukilinganisha na mabingwa wapya wa Hispania, Real Madrid, lakini Manchester United ndio klabu tajiri zaidi duniani.
Baada ya kuweweseka tangu kuondoka kwa kocha wao mkongwe, Alex Ferguson na kuwajaribu David Moyes na Louis van Gaal bila mafanikio ya kuridhisha kwenye soka na nje ya dimba, sasa United wanakuja.
Wamemaliza msimu wa 2016/17 chini ya kocha maarufu na mwenye makeke, Jose Mourinho wakiwa nje ya timu nne bora England, lakini wakafanikiwa kuingia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) watakakokwenda kupigana vikumbo na akina Real, Barcelona, Bayern Munich, Juventus na vigogo wengine wa Ulaya. Walifika huko kupitia uchochoro wa Ligi ya Europa.
Na sasa habari njema inakuja kwa jamaa wa Old Trafford, kwamba heshima imerudi mjini, kwa sababu sasa ndio klabu wanaoongoza duniani kwa utajiri, ambapo wamekutwa kuwa na utajiri wa pauni pauni bilioni 2.7, katika thamani ya kibiashara.
Taarifa iliyotolewa na kampuni ya kitaaluma ya KPMG inasema kwamba hali hiyo hupimwa kwa kutazama ingegharimu kiasi gani cha fedha kuinunua klabu ya soka, ikielezwa kwamba haki za utangazaji ni moja ya vigezo vilivyowanyanyua United.
Man U wamefanikiwa kuwapiku matajiri wa Hispania na wazuri kisoka, Real Madrid na Barcelona licha ya kwamba klabu hii inayomilikiwa na familia ya Glazer ina deni kubwa la pauni karibu nusu bilioni.
Man U wanafuatiwa, kwa utajiri wa kibiashara, na Real Madrid, Barcelona, Bayern Munich, Arsenal, Chelsea, Liverpool, Juventus, Tottenham Hotspur, Borussia Dortmund, Atlético Madrid, Schalke, Milan, Leicester, Everton, Roma, Inter, Napoli, Galatasaray, Fenerbahce, Benfica na Lyon.
Tafsiri yake ni kwamba akitokea mtu au kampuni au shirika wanaotaka kununua klabu ghali zaidi duniani itakuwa ni Manchester United.      

No comments:

Post a Comment