Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, June 1, 2017

ARSENE WENGER ATAMANI UBINGWA BAADA YA KUSAINI MIAKA MIWILIMENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amelenga kutwaa Ubingwa wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, Msimu ujao mara baada ya Leo kuthibitika amesaini Mkataba Mpya wa Miaka Miwili kubakia Klabuni hapo.
Mkataba huu, ambao hauna Kipengele cha Kuvunjwa, utamfanya Wenger adumu Arsenal kwa Miaka 23. Mara baada ya Arsenal kutangaza kusainiwa kwa Mkataba huu, Wenger alitamka: “Naipenda Klabu hii na naangaza ya baadae kwa matumaini makubwa na msisimko mkubwa!”

Habari za ndani ya Arsenal zimedokeza kuwa Wenger atapewa Kitita cha Pauni Milioni 100 kusaini Wachezaji Wapya kwenye Dirisha la Uhamisho linalofunguliwa Julai 1.

Msimu huu uliokwisha hivi karibuni, Arsenal walimaliza Nafasi ya 5 kwenye EPL na hivyo kukosa kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao kwa mara ya kwanza kwa Miaka 20 tangu 1996 Wenger aliposhika hatamu. Msimu ujao Arsenal watacheza UEFA EUROPA LIGI nafasi ambayo wameiwini mara 2 kwa kumaliza Nafasi ya 5 kwenye Ligi na pia kutwaa FA CUP walipowachapa Mabingwa Wapya wa EPL Chelsea 2-1 kwenye Fainali iliyochezwa Wiki iliyopita.
Licha kuwepo wasiwasi kuwa Wenger hatabaki Arsenal baada ya Mkataba wake kumalizika Juni hii, na hasa kusakamwa na Mashabiki wakitaka ang’oke, Bodi ya Arsenal, ikiongozwa na Mmarekani Arsene Stan Kroenke mwenye Hisa Aslimia 67, walitaka abaki.
Akiongea baada ya kuthibitishwa Wenger, Kroenke alinena: “Tunataka kutwaa Mataji, hilo ndio Mashabiki wanataka, Wachezaji, Wafanyakazi, Meneja na Bodi, wanataka na Wenger ndie bora kwa hilo!”
Nae Tajiri toka Russia, Alisher Usmanov, anaemiliki Hisa Asilimia 30 na ambae Wiki iliyopita alitoa Ofa ya Pauni Bilioni 1 kununua Hisa za Kroenke ametoboa kuwa anafurahi Wenger anabaki lakini anataka Bodi na Mmiliki Mkuu wa Hisa wamsapoti.
WENGER – HIMAYA YAKE:

-Kwenye Misimu yake 9 ya kwanza kuanzia 1996, Wenger alishinda Mataji Matatu ya EPL na FA CUP 4. -Msimu wa 2003/04, Wenger aliweka Rekodi ya kuwa Meneja wa kwanza kumaliza Msimu mzima bila kufungwa hata Mechi moja kwenye Ligi ya juu England.
-Lakini, baada ya kutwaa FA CUP Mwaka 2005, ukame ukatanda na akakaa Miaka 9 bila Kombe hadi 2014 alipotwaa FA CUP.
-Arsenal hawajakuwa Mabingwa wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, kwa Miaka 13.