Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 29, 2017

Man City waanza fujo kumwaga mamilioni



Image result for Bernardo Silva
MANCHESTER, England
MANCHESTER City wameanza fujo  za usajili kwa kumpandisha ndege, kumfanyia majaribio na kumsajili kiungo mshambuliaji wa Monaco,  Bernardo Silva.
Katika dili la pauni milioni 43.6, Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameanza kuonesha ni aina gani ya kikosi anachokitaka kwa msimu wake wa pili hapo Etihad, akiwa amemaliza huo wa kwanza pasipo kupata kikombe chochote.
Amemchukua kiungo huyu mwenye umri wa miaka 22 baada ya kuwa amemsajili kinda mwingine Gabriel Jesus kwenye eneo la ushambuliaji katikadirisha dogo la Januari, ambapo alionesha kana kwamba alitaka kumweka kando Sergio Aguero.
Hata hivyo, sasa amesema kwamba bado Aguero yumo kwenye mipango yake msimu ujao, ikielezwa kwamba mpango ni kuachana na wachezaji wenye umri mkubwa na wasio na ufanisi kadiri ya 10.
Silva ni raia wa Ureno anayecheza kwa nguvu na yumo kwenye kikosi chaTimu ya Taifa ya Ureno.
 Baadhi ya wachezaji wanaoondokani Jesús Navas, Gaël Clichy, Willy Caballero na Bacary Sagna. Wengine walio kwa mkopo pia waweza kuwa mwisho wao hapo City, nao ni Samir Nasri, Joe Hart, Eliaquim Mangala na Wilfried Bony.
Manchester City wataendelea kumwaga noti kuwanasa beki wa pembeni wa England na Tottenham Hotspur, Kyle Walker na mlinzi wa Monaco, Benjamin Mendy.

No comments:

Post a Comment